TIB YARAHISISHA UKUSANYAJI KODI SAA 24

Abraham Ntambara
BENKI ya TIB Corporate imesema tangu kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mei 16 mwaka huu ya kukusanya kodi kwa masaa 24 kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kujitokeza kulipa kupitia tawi lao dogo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo ndani ya Bandari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TIB  aliwataka wanchi kuendelea kulipia kodi kupitia benki hiyo. Alisema hilo linaenda sambamba na agizo alilotoa Rais John Magufuli kuzitaka taasisi husika katika bandari kutoa huduma siku zote kwa masaa 24.
“Benki ya TIB Corporate inawawezesha wananchi wote kulipia kodi za aina mbalimbali pamoja na tozo zote za bandari. Benki imejipanga vyema ili kuhakikisha huduma hii inaleta ufanisi na urahisi zaidi kwa mlipaji,” alisema Nyabundege.
Aidha alibainisha kuwa hivi karibuni benki hiyo iliingia mkataba na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ujulikanao kama TAXBANK.
Nyabundege alifafanua kwamba kupitia mfumo huo, mlipa kodi akilipia katika tawi lolote la benki, taarifa zake zinaonekana mara moja katika mtandao wa TRA hivyo kumuwezesha mlipa kodi kuendelea na taratibu zingine kwa haraka zaidi.
Alisema benki ya TIB Corperate ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za mamlaka ya Bandari TPA hivyo mwananchi anapolipia tozo yoyote ya bandari taarifa zake taarifa zake zitaonekana kwenye mtandao wa TPA ambazo zitarahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine.
Aidha alisema wapo katika mpango mkakati wa kujitanua na kutoa huduma kama hiyo kwenye bandari nyingine nchini ambapo alibainisha kuwa wanatarajia kwenda kwenye bandari za Mtwara na Tanga kwa ajili ya ukusanyaji wa kodi.
Aliongeza kuwa ni malengo yao pia kuweka ofisi zao nje ya nchi kama Kongo, Zambia na Uganda ambazo zitakuwa zikitoa huduma hiyo na kuahakikisha mapato ya nchi yanakusanywa pasipo kuleta usumbufu kwa mlipaji.
Aliwataka wananchi wanaohitaji huduma hiyo kutokuwa na hofu kwani wanaweza kufika wakati wowote na kuhudumiwa tofauti na awali ambapo ofisi zilikuwa zikifungwa saa 12 jioni.

mwisho
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA