Bossou Naye Atangaza Kusaini Simba


SIKU chache baada ya Haruna Niyonzima na Donald Ngoma kudaiwa kuondoka Yanga na kuwa mbioni kumalizana na Simba, beki kisiki Mtogo, Vincent Bossou naye amewaita Wekundu hao wa Msimbazi akidai yupo tayari kusaini mkataba katika kikosi chao kama wakimfuata.

Bossou aliyebeba makombe mawili ya Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga iliyo chini ya Mzambia, George Lwandamina, mkataba wake unaelekea kumalizika, jambo ambalo linamfanya awe mchezaji huru.

Akizungumza na Championi Jumatatu kutoka Togo alipo kwenye mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi, Bossou amesema kuwa kuhamia Simba kwake hakuna kitu kipya kwani maisha ya kimpira ndivyo yalivyo kwa mchezaji yeyote kuhama.

“Bado sijazipata taarifa za Simba kutaka huduma yangu kwenye kikosi chao kwa msimu ujao, lakini kama itakuwa kweli nawaambia kwamba waje tuzungumze kwa sababu mkataba wangu na Yanga unaenda ukingoni hapa, zimebaki siku chache pekee.

“Nikwambie tu kuwa hata kama itatokea nimehamia Simba kutakuwa hakuna jambo jipya kwa sababu huo ndiyo mpira, unakuta leo mchezaji yupo hapa kesho yupo kule, itategemea tu na maslahi utakayopewa,” alisema beki huyo aliyeshiriki michuano ya Kombe la Afrika (Afcon) Januari, mwaka huu akiwa na Togo.
Said Ally | CHAMPIONI| Dar es Salaam
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)