Diamond kataja moja ya vigezo vya kujiunga na familia ya WCB


Mwimbaji staa wa Bongofleva kutoka WCB Diamond Platnumz amefunguka kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM na kusema kuwa sifa ya kwanza ya WCB ni kumtoa msanii kwenye hali ngumu ili waweze kufanikiwa wote kwa kuwa huwa na adabu na kujituma.
Diamond amesema kuwa wengi wanaotoka katika familia a kitajiri wanakuwa hawana adabu kwa kuwa wanajua kwao kuna hela hivyo hawawezi kujituma ndiyo sababu WCB huchukua watu kutoka familia za chini ili wawashike mkono na wao waweze kusaidia ndugu zao.
>>>“Kweli sifa ya kwanza WCB ni kutoa msanii ambaye ametoka kwenye familia ya chini – kwenye hali ngumu na maisha magumu kwa sababu sisi tunajitahidi kujiajiri wenyewe kwa wenyewe kutengeneza riziki japo muziki wetu haujawahi kuwa na riziki. Hivyo at list kidogo hiki tule wote.
“Kwa sababu tunaamini watu kutoka mtaani wanakuwa na vipaji vya kweli. Wanakuwa na njaa ya kujituma, wanakuwa na nidhamu na wanaogopa wasije kurudi tena katika mtaa lakini watoto wa kitajiri wanakuwa hawana nidhamu kwa kuwa wanajua kwao wana hela. Kwa hiyo, yeye haogopi kufanya kazi kwa bidii anajua hata asipofanya hivyo baba yake ana hela, akifa atarithi mali zake zote.
“Kwa hiyo, sisi tunaamini sana kwamba, wale wameshafanikiwa. Ni mara kumi sisi tukatumia nafasi hii kusaidia ndugu zetu wa mtaani kwa sababu wapo wengi wanaohitaji sisi tuwashike mkono nao wafike sehemu fulani. Kesho na kesho kutwa waje kuwasaidia ndugu zao.” – Diamond
Lavalava, Msanii mpya wa WCB kwenye Interview na Millard Ayo (video)


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.