4x4

HABARI MPASUKOOO!!! Shabiki Wa Yanga, Ally Yanga Afariki Dunia Ajalini


Shabiki mkubwa wa Yanga, Ally Yanga enzi za uhai wake.
Taarifa zilizoifikia Global Publishers hivi punde zinaeleza shabiki mkubwa wa Yanga, maaruffu kwwa jina la Ally Yanga amefariki dunia.
Gari aliyopata nayo  ajali Ally Yanga huko Mpwapwa mkoani Dodoma.
Taarifa zinaeleza, Ally Yanga amefariki dunia katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amethibitisha kwamba ajali hiyo imetokea leo mchana na Ally amepoteza maisha.
Ally Yanga anakumbukwa kutokana na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa inacheza.
Alipenda kujipaka masizi meusi huku akiweka kitambi cha bandia.
Mbali na kuisapoti Yanga, alikuwa ni shabiki mkubwa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambapo mara kadhaa alisafiri na timu kwa ajili ya kwenda kuishangilia, pia katika michezo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar alikuwa akiongoza maelfu ya mashabiki kuwaunga mkono Taifa Stars.
Post a Comment