Jinsi Dominica, Barrick Gold Walivyojadili Upya Mkataba wa MakinikiaSERIKALI ya Jamhuri  ya Dominica na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Gold ya Canada nao walifanya mazungumzo kumaliza mgogoro kuhusu mkataba wa makinikia kama Tanzania.
Habari kutoka Santo Domingo zinasema Rais wa Dominica, Danilo Medina, mwaka 2013 alisema kwamba  mkataba huo una hasara kwa nchi hiyo iliyoko eneo la Carribean na kwamba ujumbe wa kampuni ya Barrick umewasili nchini humo ili kufanya majadiliano mapya ya pamoja.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Prof. Thornton
Serikali ilisema kwamba inataka mkataba huo ujadiliwe upya kwa faida ya pande zote mbili.
Mamlaka za ushuru nchini humo zilishikilia  kilo 1,264 za makinikia ambazo zilikuwa zisafirishwe kwenda nje na kampuni Barrick.  Makinikia hayo yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. Billioni 49 (Dola Millioni 22 za Marekani) yalikamatwa kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa Las Americas, mashariki mwa jiji la Santo Domingo.
Dominica imekuwa ikiishutumu Barrick kwa kufanya udanganyifu wakati wa kujaza fomu za usafirishaji wa vitu mbalimbali nje ya nchi.
Kwa upande wake, kampuni hiyo ya Canada imesema imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Dominica kwa kufuata taratibu zote ambazo bidhaa zote zimekuwa zikikaguliwa na kupitishwa na mamlaka husika za ushuru.
Kampuni hiyo inaendesha shughuli zake katika mgodi wa dhahabu wa Pueblo Viejo katika mji wa Cotui, moja ya migodi mikubwa zaidi duniani ya dhahabu.  Kampuni hiyo inamiliki asilimia 60 ya mradi huo na ndiyo inaendesha shughuli zote katika mgodi huo ambapo uzalishaji wa kibiashara ulianza Januari 2013.  Kampuni la Goldcorp la Canada linamiliki asilimia 40 ya hisa zilizobaki.

Mnamo Machi mwaka huu, mamlaka za ushuru zilisimamisha usafirishaji wa makinikia  wa Barrick kwenda nchi za nje kutokana na madai ya kuvunja taratibu za ushuru.  Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Medina kudai hadharani  kwamba kampuni hiyo lazima ifanye majadiliano mapya kuhusu mgodi wa Pueblo Viejo ambao ulikuwa hauendani na maslahi ya nchi hiyo.

 


0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)