JPM APIGA MARUFUKU WANAFUNZI WENYE MIMBA KUENDELEA NA MASOMO

RAIS John Magufuli amepiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba kuruhusiwa kwendelea na masomo.

Agizo hilo amelitoa leo alipokuwa akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Msata-Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais amesema kuwa katika katika kipindi cha urais wake hatoruhusu wanafunzi wenye mimba na waliozaa kuendelea  na masomo akihofia hali hiyo inaweza kuwahamasisha wanafunzi wengine kupata mimba.

Alizitaka NGO'S zinazohamasisha jambo hilo haziitakii mema Tanzania, na endapo wanataka mambo hayo yaendelee basi waanzishe shule zao za kuwafundisha wanafunzi waliozaa.

Pia aliimpongeza Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete kwa msimamo wake  akiwa bungeni Dodoma kupinga wanafunzi wanaopata mimba kuendelea na masomo.

Rais Magufuli alisema kwamba, hawezi kutumia sh. bil 18 zinazotengwa kila mwezi kugharamia wanafunzi, zitumike kuwagharamia wenye mimba ambao wamejitakia kwa kuendekeza ngono. Wanafunzi ambao hawataendelea kuendelea na masomo wakiwa na mimba ni kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.