Maswali 10 Unayotakiwa Kumuuliza Mtu Unayetaka ‘Kudate’ Naye!


WIKI hii nitazungumzia maswali 10 ambayo unatakiwa kumuuliza mtu unayetaka kudate naye ili majibu yake yakupe mwanga wa kinachoweza kutokea ndani ya uhusiano wako.
UPO SINGLE AU NI MTALAKA?
Unapoanza uhusiano mpya na mtu, moja ya swali unalotakiwa kuu
liza ni je, yupo single? Maana unaweza kujikuta unaanzisha uhusiano na mtu ambaye yupo kwenye uhusiano. Lakini pia kujua kama ni mtalaka au la pia ni vyema kwani hapo itakuwa rahisi kujua jinsi ya kuishi naye, kama ni mtalaka kujua pia sababu ya kuachana na mwenza wake ni vyema.
ANAFANYA KAZI GANI NA WAPI?
Kujua mtu unayetaka kuingia naye kwenye uhusiano anafanya kazi gani ni jambo muhimu sana kwani unaweza kuingia kwenye uhusiano na mtu asiyefaa kutokana na kazi anayoifanya.
KITU GANI HASA ANAKIPENDA?
Ni vema pia kujua kitu anachokipenda ni kipi, unaweza kuingia kwenye uhusiano na mtu ukakuta kumbe hobi zake na zako ni tofauti kabisa, lakini ukijua mapema itakusaidia kuamua kuwa naye kwenye uhusiano ama la.
ANAHITAJI URAFIKI AU UHUSIANO WA KUDUMU?
Kitu kingine ambacho unatakiwa kumuuliza huyo unayeanza ku-date naye ni je, anahitaji urafiki au uhusiano wa kudumu? Kwa maana unaweza kuamua kuwa naye kwenye uhusiano wa kudumu lakini akawa si mtu wa maisha bali yeye anapita tu kwako, hilo unatakiwa kuwa nalo makini. ELIMU YAKE VIPI? Kujua kiwango cha elimu yake pia ni muhimu sana, unaweza kujikuta unaingia kwenye uhusiano na mwanaume au mwanamke ambaye hana elimu, hiyo itakukosti kwa kiasi kikubwa.
ANAPENDA WATOTO/ FAMILIA?
Hili pia ni moja ya maswali ambayo unatakiwa kumuuliza kabla hamjaingia kwenye uhusiano kwani wanawake au wanaume wapo ambao hawapendi kabisa familia wala watoto. Wakati mwingine muda unakuwa haujafika lakini wengine ni matakwa yao tu.
AFYA YAKE IKOJE?
Ni muhimu pia kujua afya yake ikoje kwani unaweza kuingia kwenye uhusiano na mwanaume ama mwanamke ambaye ana historia ya magonjwa ya kurithi. Hili wapo watu wanaolifuatilia ingawa kwenye mapenzi ni ngumu, lakini pia ni vema kupata historia hiyo kwa sababu hata ukimzaa mtoto akawa na tatizo unajua limeanzia wapi.
MARAFIKI ZAKE NI WA AINA GANI? Ni muhimu
pia kujua ana marafiki wa aina gani, unaweza kuingia kwenye uhusiano na mwanaume ama mwanamke ambaye marafiki zake hawaendani na wewe kabisa ukajikuta urafiki wenu unadumu kwa muda mfupi tu.
ANAVUTA SIGARA? ANATUMIA KILEVI?
Kujua kama anavuta sigara au anatumia kilevi gani ni muhimu kwani kuna familia ambayo haipendi kabisa mambo hayo, malezi au imani zao ni tofauti na starehe hizo. Unaweza ukawa umempenda kwa mara ya kwanza tu mlipokutana, jaribu kutafuta tabia nyingine alizonazo kwenye maisha yake zilizo ndogondogo ili usije kujikuta unajilaumu. Ndiyo maana haya maswali kabla ya kuingia kwenye uhusiano yana umuhimu mkubwa.
Ni vema kujua mpenzi wako mtarajiwa anapenda vitu gani kwenye uhusiano wake kabla hamjaingia kiundani zaidi kwenye uhusiano. Haya ni miongoni mwa maswali mengi ambayo ni vema ukamuuliza mtu kabla ya kuingia naye kwenye uhusiano maana yatakuwa ni ufunguo.
ANAPENDA VITU GANI KWENYE UHUSIANO
Ni vema kujua mpenzi wako mtarajiwa anapenda vitu gani kwenye uhusiano wake kabla hamjaingia kiundani zaidi kwenye uhusiano. Haya ni miongoni mwa maswali mengi ambayo ni vema ukamuuliza mtu kabla ya kuingia naye kwenye uhusiano maana yatakuwa ni ufugoo wako.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.