MSUVA SAFARI YA KUONDOKA YANGA IMEIVA SASA NI TIMU TATU KUTOKA NCHI TATU


Timu tatu kutoka katika nchi tatu, sasa zinataka kumsajili kiungo wa pembeni wa Yanga, Simon Msuva.

Timu hizo zinatokea katika nchi za Morocco, Misri na Afrika Kusini na Msuva amethibitisha hilo.

Akizungumza na SALEHJEMBE, amesema tayari ofa hizo zimetua mezani Yanga na yeye ana taarifa.

“Nina tarifa nao na klabu inajua, hivyo ni suala la makubaliano kati yao na klabu na kati yao na mimi,” alisema.

Alipoulizwa katika ofa hizo tatu angependelea kwenda wapi kati ya Morocco, Misri au Afrika Kusini, alijibu.

“Hapa ni suala la ofa tu, nitaangalia timu na maslahi. Hivyo ni suala la kusubiri tu,” alisema.

Msuva amemaliza Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 14 sawa na Abdulrahman Mussa na wote mwisho wameibuka wafungaji bora.


Kijana huyo wa Kitanzania amekuwa akionyesha juhudi kubwa katika misimu minne mfululizo sasa hali inayoonyesha kuzivutia timu kadhaa za nje ya Tanzania.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI