Mtendaji asimamishwa kazi Kongwa


Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi ameagiza ofisi ya mkurugenzi wilayani humo kumsimamisha kazi mtendaji wa kata ya Kibaigwa Felician Ishengoma kuanzia June 14/17 kutokana na kudaiwa kukosa uaminifu na fedha za serikali.

Ndejembi akiwa katika kikao cha maandalizi ya kupokea mwenge wa Uhuru alitoa maamuzi hayo kufuatia sintofahamu ya maelezo ya mchango wa fedha taslim 600,000/=za maendeleo zilizochangwa na Kiwanda cha Kahama oil Mills kilichopo katika kata hiyo.

Kadhalika Ndejembi alieleza kuwa katika kikao km hicho cha June 8/17 Bw. Ishengoma alieleza kiwanda hicho kilichowekeza takribani bilioni 2 kimetoa mchango sh.400,000/= .

Ndejembi alibaini taarifa za Mtendaji huyo kutokuwa za uaminifu baada taarifa alizopokea kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa kiwanda hicho hivi karibuni alipotembelea kukagua ujenzi huo na katika maongezi mbalimbali aliambiwa na msimamizi huyo kuwa Kiwanda kilimkabidhi Mtendaji huyo 600,000/= kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Kongwa.

Ambapo ndejembi alilazimika kumhoji Bw.Ishengoma katika siku hiyo alipotoa agizo hill kuhusiana na ukweli wa mchango huo mbele ya wajumbe wa kikao hicho na mwandishi wa gazeti hili akiwepo Mtendaji huyo alitoa maelezo mengine tofauti na ya kikao cha awali.

"Nililikabidhiwa sh 900,000/= na Kiwanda hicho sio laki 600,000/=" Ishengoma alieleza.

Hata hivyo Ishengoma alitoa vielelezo(risiti) vya sh.300,000/= Tofauti na sh.400,000/= iliyodaiwa kukabidhiwa kwa mhasibu wa halmashauri bw.Solanus Komba.

Kutokana na sintofahamu hiyo Ndejembi aliagiza Mtendaji huyo asimamishwe kupisha uchunguzi
na tayari jukumu hilo aliwakabidhi ofisi ya Takukuru wilayani humo na wakikamilisha zoezi hilo hatua zingine zitafuata.

Pia alitoa rai kwa watendaji wote wa serikali kuhakikisha wanakuwa waaminifu katika michango wanayoipokea kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

                        Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI