MTU MMOJA AFA KWA KUIGONGA TRENI DARAJA LA MATUMBI-BUGURUNI DAR

Ajali Daraja la Reli Tabata Matumbi:

Jana kumetokea ajali ya mtu kuigonga Treni na kupoteza maisha huku mwingine akinusurika baada ya kuning'inia kwenye vyuma vya Daraja la Reli eneo la Tabata Matumbi. 

Daraja hilo la treni hutumiwa pia na watembea kwa miguu wakazi wa maeneo hayo kuvuka mto Msimbazi ambapo hakuna daraja la kawaida la watembea kwa miguu. 

Katika ajali hiyo watu wawili mwanamume na mwanamke walikuwa wakitembea kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili ambapo walipofika Darajani hapo treni ya abiria ya jiji (Dar City Train) au maarufu kwa jina la "Treni ya Mwakyembe" nayo ilikuwa inakuja kuvuka kwenye daraja lake.

Bahati mbaya na pengine kwa uelewa mdogo watu hao waliamua nao kuingia Darajani ili wapishane nayo hapo hapo juu ya Daraja. Dereva wa treni alipiga honi ya tahadhari akiamini wataondoka Darajani kuipisha lakini nao waliingia ili kupishana nayo humo humo ndipo ikawakuta na mmoja wao 
yule mwanamke akaigonga treni na kupoteza maisha papo hapo kwa kukanyagwa huku yule mwanaume akinusurika baada ya kuning'inia nje kwenye vyuma vya Daraja ili kujinusuru. 


Ifahamike kwamba daraja hilo la njia ya treni ndilo linalounganisha maeneo ya Tabata Matumbi na Buguruni Kwa Myamani, daraja hili pia ni njia ya watembea kwa miguu na chini ni mto Msimbazi. 

Mara kadhaa watembea kwa miguu hukumbana na treni wanapopita hapo Darajani na hivyo maamuzi ya haraka huwa ni kujitupa au kujitosa chini mtoni ili kuyanusuru maisha na wengi wao kupata majeraha makubwa. 

Ipo haja Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam na Serikali kwa ujumla kusikia kilio cha wakazi wa Tabata Matumbi na Buguruni Kwa Myamani ili wajengewe daraja mbadala kuwaepusha na ajali katika daraja la treni. 

Wananchi pia wamekuwa na uelewa mdogo wa kutochukua tahadhari kwenye maeneo hatarishi. Hususani yaliyo karibu na njia ya Reli. Baadhi ya wananchi huamini kuwa treni hutosha kwenye eneo la Reli yake hivyo imekuwa kawaida treni inapopita basi hutaka kupishana nayo kwa karibu sana wakiachia sentimeta chache kutoka kwenye njia ya Reli au kupanga biashara zao karibu sana na njia ya Reli bila kujua kuwa njia ya Reli ni sehemu ya ndani ya treni. Na hujikuta wakiigonga nao kuumia au kupoteza maisha. 

Kulingana na sheria za reli shughuli za watu zinapaswa kuwa umbali wa mita 30 hadi 60 kutoka ilipo njia ya Reli. Hivyo ni vema wananchi wakajua kuwa treni sio bodaboda au bajaj kwamba unaweza kujifanya 'born town' ukapishana nayo vile utakavyo. Itakula kwako na utahesabika wewe ndio umeigonga.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA