4x4

UEFA: Fainali ya Juventus na Real Madrid hatumwi mtoto dukani

Jumamosi ya leo kwa wapenzi wa soka duniani ni siku muhimu sana wakiwa wanasubiria masaa kadhaa yapite waweze kutazama mchezo wa kukata na shoka wa fainali ya michuano ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya (UEFA).
Mechi hiyo itawakutanisha kati ya Juventus ya Italia dhidi ya Real madrad ya Hispania katika uwanja wa kimataifa wa Cardiff, Wales.
Wakati mechi hiyo inaelekea kuchezwa timu zote mbili tayari zimeshafanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu katika nchi zao. Madrid ni bingwa wa La liga kwa msimu huu nao Juventus wameendeleza ubabe katika ligi ya Serie A kwa kubeba tena kombe hilo mfululizo kwa msimu huu.


Picha ya uwanja wa Cardiff, Wales ambao utafanyika mechi ya fainali ya Uefa kati ya Juventus na Real Madrid
Lakini pia ikumbukwe tayari timu hizi zimewahi kukutana katika hatua ya fainali ya kombe hili, hiyo ilikuwa ni mwaka 1998 ambapo mchezo huo ulifanyika mjini Amsterdam nchini Uholanzi. Katika mchezo huo Madrid waliibuka kidedea baada ya kuipiga Juve kwa goli moja kwa bila lililofungwa na Predrag Mijatović katika dakika ya 66.
Swali linabaki kwa mashabiki, je Madrid inayofundishwa na Zinedine Zidane kwa sasa wataendeleza ubabe wao kama uliofanywa na wachezaji waliopita kwa Juve, au timu hiyo inayoongozwa na kocha Massimiliano Allegri itavunja mwiko huo?
Post a Comment