KAJUNA, TRY AGAIN ‘MABOSI WAPYA’ SIMBA SC


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC kilichokutana jana, kimewateua Iddi Kajuna na Salim Abdallah kuwa viongozi wakuu wa muda wa klabu baada ya Rais, Evans Elieza Aveva na Makamu wake, Geoffrey Hiriki Nyange ‘Kaburu’ kuwekwa rumande kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo utakatishaji wa fedha
Taarifa ya Kaimu Katibu Mkuu, Hamisi Kisiwa kwa vyombo vya Habari leo, haijasema nani atachukua nafasi gani, lakini habari za nani zinasema Abdallah ‘Try Again’ anakuwa Kaimu Rais na Kajuna anakuwa Kaimu Makamu wa Rais.
Wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji Simba ni Collins Frisch, Said Tuliy, Ally Suru na Jasmine Costa ambao ni wa kuchaguliwa na Zacharia Hans Poppe, Mohammed Nassor, Kassim Dewji na Musley Ruweih ambao ni wa kuteuliwa. 
Salim Abdallah 'Try Again' (kushoto) akiwa na Said Tuliy (kulia)

Aveva na Makamu wake, Kaburu Juni 29, mwaka huu walipelekwa mahabusu hadi Julai 13, mwaka huu baada ya kunyimwa dhamana kufuatia kusomewa mashitaka matano Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
Wawili hao walifikishwa mahakamani mapema asubuhi ya siku hiyo na kusomewa mashitaka hayo matano mchana, ambayo ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodai kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni Rais Aveva na Makamu wake, Kaburu kiasi cha dola za Kimarekani 300,000.
Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwenye benki ya CRDB tawi la Azikiwe mjini Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sharia, ambapo inadaiwa Rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.
Shitaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka kwenye benki ya  Barclays tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu aliyemsadia Aveva kutakatisha fedha katika Barclays baada ya kughushi nyaraka.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali, Christopher Msigwa, washitakiwa hao walikana mashitaka yote na kupelekwa rumande hadi Julai 13, mwaka huu huku wakinyimwa dhamana.
Wawili hao walipandishwa kizimbani jana baada ya juzi kukamatwa na Maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi juu ya tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutokana na mchezaji Emmanuel Okwi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.