4x4

PROFESA JAY: WAKONGWE NANYI OENI SASAJoseph Haule ‘Profesa Jay na mkewe Grace Mgonjo.

WAKATI jana akiangusha pati ya kukata na shoka kwa wapigakura wake, Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ambaye pia ni rapa mkali Bongo, amewataka mastaa wakongwe nao waoe kwani ndiyo Mungu anawapa baraka zaidi.

Profesa Jay ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na mchumba’ke wa siku nyingi, Grace Mgonjo aliliambia Wikienda kuwa, kama wakongwe hao wameshajitathmini, wanawapenda na kuwaheshimu wenza wao, basi ni wakati wao sasa kukabidhi mapenzi yao mbele za Mungu.

“Nawasihi wakongwe ambao hawajaoa nao waoe kwani pale wanapokabidhi mapenzi yao mbele za Mungundipo baraka zaidi na neema za Mungu zinaambatana nao katika maisha yao yote kwa sababu ndoa ni furaha na amani pia,” alisema Jay.
Post a Comment