Tarehe
14 Julai, 2017 ilikuwa ni siku ya Tanzania Jijini Ottawa, Canada. Siku
hii ilikuwa ni mwendelezo wa sherehe za kuazimisha miaka 150 ya uwepo wa
Taifa la Canada. Mamlaka ya Jiji la Ottawa ilitoa fursa kwa ofisi
mbalimbali za kibalozi kushiriki katika sherehe hizo ambazo zimekuwa
zikiendelea tangu Januari 2017. Tarehe 14 Julai ilipangwa kwa ajili ya
Tanzania. Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Ottawa ulitumia siku hiyo
kuitangaza nchi yetu katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, utalii
na utamaduni.
Balozi
wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka akijiandaa kukata utepe ili
kuzindua siku ya Tanzania Jijini Ottawa, Canada. Kulia ni mke wa Balozi
Bi. Esther Zoka na kushoto ni afisa wa Ubalozi Bi. Aisha Mandia akiwa
ameshika "tray" iliyokuwa na mkasi.
Mhe.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Jack Zoka akiwa na mke wake Bi. Esther
Zoka, akikata utepe kuashiria kuanzishwa kwa shughuli mbalimbali
zilizofanyika siku hiyo.
Mhe. Balozi Jack Zoka akiwa na Meya wa Jiji la Ottawa Bw. Jim Watson na Bi. Esther Zoka
Bi.
Petronilla Lyimo, Mshereheshaji wa siku hiyo ambaye ni mke wa Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Wana-diaspora wa Tanzania Jijini
Ottawa (TAO)
Mhe. Balozi Jack Zoka akimtembeza Meya Jim Watson kwenye maonyesho ya vikundi mbalimbali vilivyoshiriki siku hiyo.
Afisa
wa Ubalozi Bw. Leonce Bilauli akitoa zawadi kwa Meya wa Jiji la Ottawa
Jim Watson alipotembelea ukumbi wa maonyesho akishuhudiwa na Balozi wa
Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka.
Wakiwa
katika picha ya pamoja, Meya Jim Watson akiwa na Mhe. Balozi na Afisa
wa Ubalozi Bi. Fortunata Ngoli. Kushoto ni Mke wa Balozi Bi. Esther
Zoka.
Afisa wa Balozi Bi. Aziza Bukuku akiwa kwenye banda la Ubalozi akielezea wageni kuhusu Tanzania
Mhe.
Balozi Jack Zoka na Bi Esther Zoka wakiwa na mgeni rasmi kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje ya Canada Bw. Mark Mostovak wakati wa hafla iliyofanyika
jioni.
Balozi wa Tanzania nchini Canada akitoa hotuba wakati wa hafla iliyofanyika jioni
Mgeni rasmi Bw. Mark Mostovac akitoa hotuba kwa niaba ya serikali ya Canada wakati wa halfa ya jioni
Bendi ya "Hapa Kazi tu" wakichangamsha wageni mbalimbali waliofika kujionea na kusikiliza kuhusu Tanzania
Comments