Bunge la Afrika Kusini limeshindwa tena kumuondoa Rais Zuma


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini leo August 8, 2017 amenusuria kwa mara nyingine jaribio la kuondolewa madarakani baada ya Bunge la nchi hiyo kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani naye.
Kufuatia mjadala mrefu na mchakato wa kupiga kura uliodumu kwa saa mbili, Wabunge 198 walipiga kura kupinga azimio la Democratic Alliance ambao walipiga kura 177 wakionesha kutokuwa na imani naye.
Aidha, Wabunge 30 wa Chama tawala cha ANC walipiga kura kutaka Zuma aondolewe ambapo ili kuondolewa madarakani zilihitajika kura 201.
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Baleka Mbete alitangaza Jumatatu kuwa kura zitapigwa kwa siri kwa mara ya kwanza tofauti mara kadhaa zilizopita ambazo kura za kutokuwa na imani na Zuma zipigwa kwa njia ya wazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI