JAFO: ZOEZI LA HOSPITALI TEMBEZI LIFANYIKE MIKOA YOTE








Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya ya Kondoa na Chemba.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya za Kondoa na Chemba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.James Kiologwe na viongozi wa wilaya ya Chemba na Kondoa.
Wananchi waliofika katika uzinduzi wa hospitali tembezi.
 ............................................................................
 
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania bara kuratibu zoezi la Hospitali tembezi katika mikoa yao ili kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kupata huduma ya kibingwa. 

Jafo ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizindua huduma za hospitali tembezi kwa wilaya ya Chemba na Kondoa zoezi ambalo limefanyikia mjini Kondoa.

Mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika katika wilaya ya Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na sasa linaendelea kwa wilaya za Chemba na Kondoa.

Akizindua huduma hiyo, Jafo ameumwagia sifa uongozi wa mkoa wa  Dodoma  kwa kuratibu vyema zoezi hilo ambapo zaidi ya wagonjwa 8,000 wamefanyiwa uchunguzi huku 500 wakifanyiwa upasuaji mdogo na mkubwa.

Amewataka wananchi wa wilaya hizo kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa huku akiwataka kupima tezi dume kwa kuwa umekuwa ugonjwa tishio kwa wanaume.
Ameeleza kuwa huduma hizo za kibingwa zinatolewa kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha wananchi wasio na uwezo kupata matibabu.

Jafo amewapongeza madaktari bingwa wa mkoa wa Dodoma kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewataka wengine waige mfano wa Dodoma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.