WAKULIMA WA MKIKITA KUKITUMIA KIWANDA CHA UKAYA KUSAGA MUHOGO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kulia) akizungumza na uongozi wa Kiwanda cha Unga wa Muhogo cha Ukaya, alipotembelea na kukubaliana kuingia mkataba wa kukitumia kiwanda hicho kusaga mihogo ya wanachama wa Mkikita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Ibrahim na Meneja wa kiwanda, Matanga Joseph. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Uongozi wa Mkikita ukiwa na uongozi wa kiwanda ulipokwenda kukagua kiwanda cha Unga wa Muhogo, Mkuranga, Pwani. Kutoka kushoto ni, Dk. Kisui, Ibrahim, Matanga na Adam.

Na Richard Mwaikenda, Mkuranga

MTANDAO wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/ Livingreen), uko mbioni kuingia mkataba wa makubaliano na Kiwanda cha usagisaji wa unga wa muhogo cha Ukaya kilichopo Mkuranga, mkoani Pwani.

Mpango huo unaandaliwa baada ya viongozi wa Mkikita kutembelea kiwanda hicho na kufanya mazungumzo ya kina na uongozi wa kiwanda hicho kinachozalisha unga wenye ubora.

Akizungumza baada ya kukikagua kiwanda hicho, Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange alisema kuwa kiwanda hicho ni ukombozi mkubwa kwa wanachama wa mtandao huo ambao wamejikita kwenye kilimo cha muhogo.Katika ziara hiyo alikuwepo pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurunzi wa Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui.

Alisema kuwa unga utakaosagwa hapo utakuwa unauzwa katika soko la ndani pamoja na la nje ambalo linauhitaji mkubwa wa nafaka hiyo. Soko la unga wa muhogo tayari limepatika katika nchi za Asia.

Akizungumzia kuhusu makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Ibrahim amesema kuwa amepata faraja kupata ugeni huo muhimu kutoka Mkikita na kwamba yupo tayari kufanya nao kazi ili kuwakomboa wakulima wa zao hilo nchini.

Alisema kuwa kiwanda hicho kilichoanzishwa mwaka 2011 katika Kijiji cha Kimbwanindi, wilyani Mkuranga kwa hivi sasa kina uwezo wa kuzalisha kati ya tani 3 na 4 kwa siku na kwamba kikiunganishwa na umeme mwezi Januari kitakuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha hadi tani 40 kwa mwezi. Hivi sasa kinatumia mafuta ya dizeli kuendeshea mitambo jambo ambalo tayari lilingiliwa na Rais John Magufuli kwa kuwaagiza Tanesco kuhakikisha wanakipatia kiwanda hicho umeme ifikapo Januari 2018.


 Matanga Joseph (katikati) akitoa maelezo kuhusu sehemu ya kuoshea mihogo baada ya kumenywa
 Dk. Kissui na Adam wa Mkikita wakioneshwa mashine ya kukatakata mihogo
 Matanga akionesha sehemu ya kukamulia maji mihogo
 Adam akiangalia mashine ya kusagia muhogo
 Matanga akionesha sehemu wanapotumia mlipuko wa dizeli unaotumika kuendeshea mashine za kusaga muhogo
 Wakionshwa sehemu ya kuwekwa vipande vya muhogo tayari kusagwa


 Stoo ya kiwanda hicho
 Sehemu ya kuanikia
Dk. Kissui akioneshwa Taasisi zinazothibitisha ubora wa kiwanda hicho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.