HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

Picha ya mchawi (Picha ya Maktaba)

Na Richard Mwaikenda, Kivule
MCHAWI kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 amedondoka leo majira ya saa 9 usiku karibu na Shule ya Msingi Misitu, Kivule, Ukonga, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo amesimulia kuwa mchawi huyo alikutwa 
eneo hilo akiwa uchi wa nyama huku akiwa hajitambui.

Anasema ilipofika asubuhi watu walianza kujazana kumshangaa huku wengine wakitishia kumpiga na wengine kumwagia mchanga.

Ili kumnusuru asidhurike, mmoja wa wazee wa eneo hilo alimsitiri kwa khanga na kumpeleka ofisi za serikali ya mtaa.

Alipofikishwa Serikali ya mtaa alihojiwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo, nini kilichomsababisha awe kwenye hali hiyo, alijibu kuwa aliachwa na bibi yake wakiwa njiani kwenda kuwanga

Kijana huyo anaeleza kuwa yeye na bibi yake walitokea Mbagala kwenda eneo hilo kuwanga lakini kwa mazingira ya kutatanisha alijikuta ameachwa eneo hilo kwa kudondoka kutoka kwenye ungo.

Hata hivyo inadaiwa baadhi ya maswali alikuwa anakataa kujibu likiwemo ni nani walikuwa wanakwenda kumuwangia na amewakosea nini.

Shuhuda aliyekuwa anasimulia tukio hilo anasema alipomuona mchawi huyo ambaye kwa rika wanalingana aliingiwa na hofu kiasi cha kushindwa hata kumpiga picha kwa simu.

Msimuliaji huyo anasema aliondoka eneo la tukio saa 3 asubuhi akimwacha mchawi eneo hilo wahusika wakijiandaa kumpeleka Kituo cha Polisi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

DK MAGUFULI AZISAMBARATISHA NGOME ZA MBOWE, NDESAMBURO NA NASSARI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

WAKIANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA, MBOZI