Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo apandishwa kizimbani


Nondo aliripotiwa kutekwa baada ya kuelezwa kuwa alituma ujumbe wa simu kuwa yuko hatariniHaki miliki ya pichaNONDO FACEBOOK
Image captionNondo aliripotiwa kutekwa baada ya kuelezwa kuwa alituma ujumbe wa simu kuwa yuko hatarini
Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo amepandishwa mahakamani leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mjini ambapo anashatakiwa kwa kosa la kudanganya kuwa alitekwa na kudaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.
Leo ni siku ya 21 tangu kushikiliwa kwa mwanafunzi huyo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya kufikishwa mahakamani kijana huyo amenyimwa dhamana na hakimu mkazi wa mahakama hiyo kwa sababu ya "usalama wake kuwa hatarini".
Imeelezwa kuwa kupewa dhamana kunaweza kuleta hatari zaidi, aidha hakimu huyo ameahirisha kesi hadi siku ya Jumatatu ili aweze kupitia vifungu vya sheria na kujihakikishia kama ni salama kumuachia kwa dhamana au la.
Wakati mwanafunzi huyo akiwa mahakamani mkoani Iringa kesi nyingine iliyofunguliwa na jopo la mawakili wake wakiongozwa na wakili Mpale Mpoki juu ya utaratibu mzima wa kukamatwa kwa kijana huyo pamoja na suala la dhamana, ilikua inaendelea katika mahakama kuu jijini Dar es salaam na kuahirishwa hadi tarehe nne mwezi wa nne ili pande zote ziwasilishe nyaraka zao.
Kesi hiyo ilifunguliwa dhidi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI), Mwanasheria mkuu wa serikali na mkuu wa jeshi la polisi IGP kwa madai ya kuchelewesha kumshtaki mahakamani mwanafunzi Abdul Nondo na kumnyima dhamana bila sababu ya msingi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.