NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

 Mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahim (wa pili kushoto) na Diwani wa Kata ya Mbezi, 
Rashid Selungwi (juu kushoto), wakiwa na wanachama pamoja na baadhi ya wanakijiji wakishangilia juu ya katapila wakati wa uzinduzi wa Mashamba Mji katika Kijiji cha Msolwa, wilayani Mkuranga, Pwani. 


Na Richard Mwaikenda, Mkuranga

Taasisi ya Namaingo Business Agents (NBA), imezindua Mashamba Mji katika Kijiji cha 
Msolwa, Kata ya Mbezi, wilayani Mkuranga, Pwani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashamba Mji, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Biubwa Ibrahim maarufu kwa jina la Bi. Ubwa, amesema kuwa eneo hilo lina ukubwa wa heka 7000 zitakazogawiwa kwa wanachama pamoja na wana kijiji.

Amesema kuwa eneo hilo litagawiwa kwa mpangilio maalumu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka kwa washirika wao Kampuni ya BlackWood Consult wanaoendelea kulisafisha na kuchonga barabara. Pia watalipima na kila mwanachama atapatiwa hati miliki.

Akizungumza huku akishangiliwa mara kwa mara Bi, Ubwa, amesema Black Wood watagawa kwa utaratibu wa mwanachama kupata eneo la makazi, shamba la kuzalisha mazao mbalimbali, ufugaji na soko.

Amesema itawekwa miundombini ya kila aina  kama vile barabara, maji, umeme hali itakayufanya mji huo kuwa wa kisasa na wa kibiashara.

Aidha Bi Ubwa amesema kuwa Mji huo utawanufaisha wanakijiji na vijiji jirani kwa kupata fursa mbalimbali za uwekezaji, kupata ushauri, kupata mbegu na utaalamu utakaowezesha kupata mazao bora.

Alitaja mazao yatakayopewa kipaumbele cha kulimwa katika eneo hilo kuwa ni pilipili, Chia, mchaichai pamoja na mazao mengine watakayoona yanafaa.

Akizungumza kwa niaba ya wanakiji, Diwani wa Kata ya Mbezi, Rashid Selungwi, alisema 
kuwa wananchi wa eneo hilo wamefurahi ujio wa mradi huo utakaowaletea maendeleo makubwa.

Kwanza alimsifu Mkurugenzi  wa Namaingo kwa kufanikisha mradi huo kufika kijijini hapo na kwamba kwa hatua hiyo anastahili kuitwa Profesa au Dk. kwani amewashinda hata wenye sifa hizo.

Naye Mwakilishi wa Wazee wa Kijiji hicho, Mzee Ali Kitasa, aliipongeza hatua hiyo ya Namaingo na kwamba wananchi wa eneo hilo hawana kinyongo wanaukaribisha mradi huo na wataupigania kuhakikisha hakuna vikwazo.

Mzee Kitasa aliongoza dua ya uzinduzi wa mradi huo na kuahidi kuwa yeyote atakayethubutu kuukwamisha basi kwa ushirikiano na Namaingo watapambana naye na kushinda kwa nguvu za Mungu.\

Namaingo ilikabidhi kwa wazee wa kijiji hicho vyakula mbalimbali ikiwemo mchele, unga, mafuta, majani ya chai, maji pamoja na mbuzi. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202







 Mzee wa Kijiji cha Msolwa, Mohamed Kitasa (wa pili kushoto) akiongoza dua ya uzinduzi huo Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Mbezi, Rashid Selungwi, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Moshi Mtandola  na  Biubwa,
 Biubwa na Selungwi wakimkabidhi vyakula Mzee Kitasa kwa niaba ya wazee wa Kijiji hicho.
 Mbuzi akichinjwa ikiashira uzinduzi
 Baadhi ya wanachama wa Namaingo akiingia kwenye shamba hilo la Msolwa
 Sehemu ya shamba hilo iliyofanyiwa usafi
 Wakiangalia shamba hilo
 Moja ya barabara zilizochongwa
 Baadhi ya wanachama wa Namaingo
 Biubwa akitoa maelezo kuhusu mradi huo
 Ni furaha kwa kwenda mbele

 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Namaingo, Ignus Augustine (kushoto) akiwakaribisha baadhi ya wazee wa kijiji hicho. Kulia ni Salum Athuman na Ali Kitasa.
 Wakishangilia
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Msolwa Moshi Mtandola akitoa neno la shukrani pamoja na kuwakaribisha wageni wanachama wa Namaingo.
 Wakimba Dua
 Baadhi ya wazee wa Kijiji cha Msolwa. Kutoka kushoto ni Shaban Ali, Ramadhan Athuman, Ali Kitasa na Salum Athuman
 Diwandi wa Kata ya Mbezi, Rashid Selungwi aktoa neno la shukrani kwa Namaingo kuupeleka mradi huo kijijini hapo.
 Mwenyekiti wa Kamati za Namaingo, Katto akitoa neno na kumkaribisha Mkurugenzi, Bi. UBWA KUZUNGUMZA
 Biubwa akimkabidhi vyakula Diwani wa Kata ya Mbezi kwa ajili ya wanakijiji

 Wanachama wa Namaingo wakiwa na baadhi ya wanakijiji cha Msolwa

 Katapila likichonga barabara katika shamba hilo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA