RAIS MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA SIGARA MANSOOR INDUSTRIES LTD KILICHOPO KINGOLWIRA MOROGORO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Sigara cha Mansoor Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip Morris Tanzania katika eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga makofi, wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha Sigara Mansoor Shanif Hirani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mapakiti ya sigara hizo za Marlboro wakati akikagua utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mara baada ya kukifungua.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda hicho mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya kukifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kutoa burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi CCM katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akipongezwa na baadhi ya wananchi mara baada ya kuimba wimbo wake wa Mimi ni Msanii katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.
Mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa  Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na wadau mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada kufungua kiwanda hicho. PICHA NA IKULU.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.