CEO ADAM AWA KIPUSA MBELE YA WAZUNGU DAR .Avuna Fursa Kibao

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (aliyevaa koti jeusi) akiwa katika hafla na  Watasha kutoka Taasisi ya LoccoZ ya Uswisi na Aquaculture ya Norwe kwenye Hoteli ya Coral Beach, Masaki Dar es Salaam jana. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;0715264202,0689425467
 Ngamange akiwa katika majadiliano jambo na CEO wa Loccoz, Ziccolillo (kushoto) pamoja na CEO wa Aquaculture, Ari.

 Mshauri wa Habari wa Mkikita, Richard Mwaikenda (kulia), akiwa na viongozi wa Loccoz, Karin na Ziccolillo kwenye Hoteli ya Coral Beach, Masaki Dar es Salaam.
 Ngamange akiwa katika majadiliano jambo na CEO wa Loccoz, Ziccolillo (kushoto) pamoja na CEO wa Aquaculture, Ari.
Ngamange akiagana na raia wa Uingereza baada ya kumaliza kufanya mazungumzo naoNa Richard Mwaikenda, Masaki.

 Ilikuwa Ijumaa Aprili 22, mwaka huu kwenye Hoteli ya Kitalii ya Coral Beach Club, Masaki, Dar es Salaam, majira ya jioni saa 11, tukiwa na CEO wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange ambaye aliwahi ahadi ya kuwaaga viongozi wa Taasisi ya LoccoZ My Solutions waliokuwa wanasafiri kurejea nyumbani kwao Uswisi baada ya kusaini makubaliano ya awali ya LoccoZ kuwajengea Mkikita Kijiji Uchumi mkoani Pwani.

Tukiendelea kuwasubiri huku tukibarizi upepo mwanana wa Bahari ya Hindi umbali wa sentimita mbili kutoka tulipokuwa tumekaa, mara akatokea  Mkurugenzi wa  Taasisi ya Aquaculture Farming Project ya Norwe, Ari akiwa na watu watatu, waafrika wiwili na mzungu mmoja wakaungana nasi tulipokaa.

Mtanzania Augustius ambaye tunafahamiana naye ambaye alikuja naye Ari alitoa utambulisho wa pande zote mbili. Baada ya hapo mazungumzo kati ya Adam na Ari yalianza kwa kuuliza kila mmoja anashughulika na nini, Ndipo Adam alianza kujitambulisha  kuwa ni CEO wa Tanzania Livinggreen Network yenye wanachama zaidi 7000 nchini ambayo kazi yake ni kutoa taarifa za kilimo (Infomation), kusimamia (Management), Uwezeshaji (Financing) na Masoko (Marketing).

Ari alifurahi sana kuelezwa hivyo ambapo na yeye alimweleza Adam kuwa taasisi yake imebobea katika Kilimo Maji (Aquaculture Farming) yaani ufugaji wa samaki, mboga mboga, matunda na vyakula mizizi, mazao ambayo yana soko kubwa katika nchi za Ulaya ikiwemo Norwe.

Kusikia hivyo Adam alistuka na haraka haraka akaanza kumuuliza Ari endapo itawezekana taasisi yake inaweza kuwekeza Mkikita, kwani tayari wana heka 250 za shamba lililo kando ya Mto wami. 

Ari hakusita alikubali ombi hilo na kwamba wataandaa utaratibu wa kuwezesha hilo na kuahidi kukutana kesho yake kuendeleza makubliano yao juu ya uwekezaji huo.

Ilipotimu saa 12.30 jioni ilitinga eneo hilo timu ya LoccoZ, CEO Giuseppe Zoccolillo na Mkuu wa Masoko, Karin Legler na watoto wao, Timo na Jan na kuja moja kwa moja eneo tulilokaa ambapo pia alikuwepo Ari, walifurahi sana kutukuta na kumpongeza Adam kwa kuwahi kama walivyokubaliana. 

Adam aliwakabidhi zawadi viongozi hao wa LoccoZ, ikiwemo fulana yenye maneno ya kiingereza yaliyotafsiriwa kwa kiswahili waliyoifurahia sana na kuahidi kwenda kuiweka kwenye ofisi yao kama kumbukumbu na kufundisha wengine lugha ya kiswahili. 

Adam aligeuka kuwa kivutio kwa wazungu hao kwani kila mmoja alitaka akae naye karibu na kuongea naye. Walipofika viongozi wa LoccoZ waliondoka kwenye viti vyao na kwenda kukaa viti walivyokuwa wamevikalia viongozi wa Aquaculture waliokuwa wamesimama pembeni wakijadiliana jambo. Walifanya hivyo ili mradi wawe karibu na Adam ambaye ni mcheshi na mara nyingi alikuwa anaongea mambo ya maana ya kusaidia jamii ya kitanzania kuondokana na umasikini.

Baada kuona viti vyao vimekaliwa na waswisi, kwa unyonge wanorwe walichukua vinywaji vyao na kujongea kwenye viti vingine ambavyo vilikuwa special kwa waswisi.

Inavyoonekana waswisi hawakupendezewa na kitendo cha wanorwe kukaa karibu na Adam kutokana na ishara zilizoonekana. 

Kabla ya kuondoka, Karin alimwambia Adam kuwa anasikitika kuondoka na kumuacha yeye ambaye kwa muda wote waliokuwa hapa nchini timu yake ilifurahi  kuwa naye pia jambo lingine ni kuikosa hali ya hewa nzuri ya Tanzania ukiwepo upepo mwanana wa Bahari ya Hindi.

Adam ambaye mei mwaka huu atafanya ziara nchini Uswisi kwa mwaliko wa LoccoZ, kwenda kusaini mikataba ya ujenzi wa Kijiji Uchumi, ameahidiwa na Karin kuwa atakapo kuwa huko hatomruhusu Adam kwenda kula Hotelini bali atakuwa anampikia chakula nyumba kwake.

"Kuanzia sasa mimi ni mtanzania, nitaifanya nchi hii ni mahali pangu pa kuishi, ina watu wazuri wenye ukarimu na hali ya hewa nzuri." alisema CEO wa LoccoZ, Zoccolillo.

Kabla ya Wanorwe kuondoka alikuja Muhudumu na kuwaeleza Waswisi kuwa wazungu raia wa Uingereza mume na mke waliokuwa wakibarizi eneo hilo wanaomba waje wakae kwenye meza yetu, bila ajizi Waswisi waliwakaribisha.

Waingereza hao wazee walikuja na kupishwa kwenye viti na Waswisi ambao wakati huo walikuwa wanajiandaa kwenda Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya kurejea kwao.

Wakati wa kuaga walimwendea Adam kumpa salamu za kwa heri huku wakimkumbatia kuonesha ishara ya upendo.

Baada ya Adam kuachwa na Waingereza, hakufanya ajizi alianza kujitambulisha na kufuatiwa na utambulisho wao. Adam alipowaambia kuwa karibu Tanzania, walijibu kuwa wao ni Watanzania Tayari kwani wanaishi Tangeru, wilayani Korogwe, Tanga na kwamba kila mwaka lazima waje Tanzania kutoka Uingereza.

Walisema moja ya kazi kubwa wanayoifanya wakiwa nchini, ni kusaidia Jamii kwa kuwachimbia visima vya maji. Walisema kuwa hadi sasa wameshatoa msaada wa ziadi ya visima 50. 

Adam aliwapongeza kwa kazi nzuri ya kusaidia jamii, lakini vile vile aliomba wafanye mpango wa kuwasaidia visima wanachama wa Mkikita, ombi ambalo walilikubali na kwamba mipango hiyo itafanyika watakaporejea kutoka Uingereza kwani siku ya pili yake walikuwa wanajiandaa kurejea kwao Uingereza. Pia walikubali mpango wa Mkikita kusimamia mashamba yao yaliyopo Korogwe.


0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA