DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

 MKUU wa Wilaya ya Mkuranga, Filbeto Sanga (kushoto) akiongoza kupanda mbegu za viazi lishe wakati wa uzinduzi rasmi Mradi wa Mashamba Mji unaoendeshwa na Taasisi ya Namaingo katika Kijiji cha Msolwa, Kata ya Mbezi, wilayani humo katika tukio lililofanyika leo.Na Richard Mwaikenda, Mkuranga

MKUU wa Wilya ya Mkuranga, Sanga ameindua rasmi Mradi wa Mashamba Mji unaoendeshwa na Taasisi ya Namaingo katika Kijiji cha Msolwa, Kata ya Mbezi, wilayani humo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Sanga aliwataka wakazi wa kijiji hicho kuichangamkia fursa hiyo muhimu kwa kujiunga kwa wingi katika mradi huo wenye manufaa makubwa kiuchumi.

Mradi huo wa Mashamba Mji wenye heka 1000 ukikamilika utakuwa wa mfano nchini, kwa vile patajengwa nyumba za kuishi sambamba na mashamba yatakayolimwa kisasa pamoja na ufugaji wa samaki.

"Mradi huu ni darasa la kujifunzia,hivyo inabidi utalaamu mtakaoupata mkaufanyie kazi kwa kulima kwenye mashamba yenu mtapata mafanikio makubwa," amesisitiza mkuu huyo wa wilaya.

Amesema kuwa ujio wa mradi huo utaisadia serikali ya awamu ya tano kupunguza tatizo la ajira katika wilaya hiyo, hivyo kuwataka vijana wa kijiji cha Msolwa kupewa kipaumbele katika uendeshaji wa shughuli za kila siku za mradi huo.

Sanga amesema kuwa hatopenda kusikia kwamba watu kutoka maeneo mengine wamepata ajira na kuwasahau watu wa kijiji hicho. Lengo ni kuwapatia kwanza ajira wakazi wa Msolwa ndipo wafuatie wengine.

Pia, kutokana na kuwepo kwa fursa ya mradi huo utakaowaongezea kipato wakazi wa Msolwa, Sanga amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wote waliotimiza umri wa kwenda shule  wakiwemo na waliofaulu msimu huu na kwamba atayethubutu kukaidi amri hiyo hatakuwa na utani wala mjadala naye bali sheria itafuata mkondo wake.

"Mwenyezi Mungu atupe nini? Atupatie umasikini?!!!, Tunashukuru sana Namaingo kutuletea fursa hii muhimu kwetu, ambayo tumezoea kufanyiwa na wazungu lakini sasa imefanywa na wazalendo, amesema Sanga huku akishangiliwa.

Mkuu huyo wa Wilaya, ambaye hata yeye amejiunga na Taasisi hiyo, alizindua kitabu kinachoelezea utekelezaji wa mradi huo utakaoendeshwa na wanachama katika shamba la pamoja (Block Farm) ambalo wameanza kupanda viazi lishe na baadaye kufuatiwa na pilipili kichaa mazao ambayo yana soko tayari lililotafutwa na Kampuni ya Vegrab Organic Farming Ltd.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahim, kwanza alimshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo, Sanga kwa kuukubali mradi huo kwa mikono miwili, ikiwemo pia kujiunga na taasisi hiyo pamoja na kuuzindua ili uanze rasmi.

Biubwa alisema kuwa Mradi huo utawasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kiasi kikubwa kwa kupata ajira na kuwa na mashamba watakayoyamiliki na kwamba kitendo hicho kitawaongezea kipato na kuwapunguzia  umasikini.

Amesema kuwa hadi sasa heka 300 zimetengwa katika block za heka mia mia na tayari baadhi ya heka zilizogawiwa kwa wanachama wameanza kupanda viazi lishe ambavyo tayari soko lake lipo nje ya nchi.

Alisema kuwa katika shamba hilo kutakuwepo na ufugaji wa nyuki utakaofikia hadi mizinga 50,000 kwa ajili ya kupata asali. Pia Namaingo itakuwa itaendesha mafunzo ya Kilimo Biashara kwa wananchi kila wiki mara mbili.

Kila mwanachama atapimiwa eneo lake na Kampuni ya Black Wood na kupatiwa hati miliki ambapo wataendesha kilimo biashara pamoja na ujenzi wa nyumba za kuishi.

Baada ya hafla hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Msolwa, Mkuu wa Wilaya, viongozi wa Namaingo na wananchi walikwenda kukagua shamba hilo ambapo pia liliendeshwa zoezi la kuwagawia mashamba wanachama.
.


 MKUU wa Wilaya ya Mkuranga, Sanga akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa shamba hilo lenye ukubwa wa heka 7000. Kutoka Kushoto ni Mzee wa Kijiji hicho, Mohamed Kitasa, Mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahim na Diwani wa Kata ya Mbezi, Rashid Selungwi. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG 0715264202,0689425467
 Sanga akikaribishwa na Biubwa alipowasili katika hafla hiyo
 WANACHAMA WA nAMAINGO WAKISHANGILIA UJIO WA mKUU WA wILAYA
 Mzee wa Kijiji cha Msolwa, Mohamed Kitasa akiomba dua wakati w hafla hiyo
 Mtaalamu kutoka Kampuni ya Vegrab Organic Farming Ltd, Josephat akielezea kuhusu kilimo cha viazi lishe na soko lake nje ya nchi. Ni kwamba kwa muda wa miezi mitatu tangu lipandwe unavuna na kupata hadi sh. mil. 5 kwa heka.
Sehemu ya wanachama wa Naimaingo
Sanga akionesha kitabu kinachoelezea utekelezaji wa mradi huo. Kulia ni Biubwa
Sehemu ya wanakijiji  wa Msolwa wakiwa katika hafla hiyo
Wakisikiliza kjwa makini wakati Mkuu wa Wilaya akihutubia


Mkuu wa Nidhamu wa Namaingo, Ignus Augustine (kulia0 akiwa na Mkuu wa Wilaya, wakielekea kukagua shamba
Wanachama wakiwa shambani tayari kugawiwa heka zao
Wakishangilia baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Sanga (wa pili kulia) kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa shamaba hilo
Wanachama wakifurahia
Mkuu wa Wilaya akikagua shamba hilo
Mkuu wa Wilaya akiongozana na wanachama pamoja na wananchi wa Msolwa kwenda kupanda mbegu za viazi lishe
Sanga akizungumza na wananchi kabla ya kuanza kupanda mbegu za viazi
Wakichukua mbegu tayari kwa kupanda
Sehemu ya sahamba hilo

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA