Kim Jong Un: Korea Kaskazini imesitisha majaribio ya silaha za kinyuklia


Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UnHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-Un, ametangaza kusitishwa kwa mda shughuli zake za kufanya majaribio ya silaha zake za Kinyuklia.
Kim Jong-Un amedai kwamba hamna haja ya kufanya tena majaribio kwa sababu nchi yake tayari imefanikiwa katika malengo yao ya kuwa wamiliki wa zana za kinyuklia
Tangazo hilo linajiria wakati kuna harakati za kuharibu kufanikisha maandalizi ya mikutano inayotarajiwa kufanyika baina ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na raia wa Marekani Donald Trump.
Je ni makombora gani yanayomilikiwa na Korea Kaskazini?
Image captionJe ni makombora gani yanayomilikiwa na Korea Kaskazini?
Katika ujumbe wa Twitter Donald Trump amepokea hatua hiyo ya Korea Kazkazini.
Lakini maswali yangali yanaulizwa -kuhusu nia halisi ya tangazo hilo la Kim Jong-Un .
Rais Donald Trump wa Marekani
Image captionRais Donald Trump wa Marekani
Msururu wa majaribio ya makombora ya kinyuklia yaliyofanywa na Korea kazkazini mwaka jana yalizua taharuki miongoni mwa majirani zake hasa Japan na Korea Kusini na vile vile mshirika wao mkuu Marekani.
Pamoja na malumbano ya maneno makali baina yao, Marekani imekuwa mstari wa mbele kuhimiza vikwazo chungu nzima vya kiuchumi huku nchi zinazokiuka vikwazo hivyo nazo zikifuatiliwa kwa karibu sana.
Ziara ya bwana Pompeo's (left) nchini Korea Kaskazini ililenga kuandaa mkutano kati ya Trump na KimHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionZiara ya bwana Pompeo's (left) nchini Korea Kaskazini ililenga kuandaa mkutano kati ya Trump na Kim
Maandalizi ya mkutano kati ya trump na Kim Jon Un yalifannikiswa na mkurugenzi wa shirika la ujasusi Marekani CIA ,Mike Pompeo ambaye aliunda "uhusiano mzuri" na kiongozi huyo wa Korea kaskazini walipokutana wiki iliyopita, kwa niaba ya Rais Trump katika ujumbe wake wa Twitter.
Akithibitisha taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari kuhusu mkutano huo wa siri mjini Pyongyang, Trump amesema mkutano ulimalizika "bila ya tashwishi".
Ziara hiyo ya kushtukiza inadhihirisha mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya Marekani na Korea kaskazini tangu 2000.
Rais Donald Trump anatarajiwa kuandaa mkutano na Bwana Kim kufikia mwezi Juni. Bado ratiba inaandaliwa, rais wa Marekani amesema.
Mkutano huo ulioandaliwa kuandaa mkutano mwengine kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un ulifanyika wikendi ya sikukuu ya Pasaka.
Bwana Trump alikuwa amekiri kufanyika kwa mazungumzo ya hadhi ya juu na Pyongayng.
''Tumekuwa na mazungumzo ya moja kwa moja , katika ngazi za juu'', Bwana Trump alisema mjini Florida ambapo alikuwa anakutana na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Rais huyo aliongezea kuwa aliunga mkono mazungumzo kati ya Korea kusini na kaskazini kuzungumzia makubaliano ya amani ya kumaliza vita vya Korea vya 1950-1953
Korea Kusini imetoa ishara kwamba itaangazia suluhu rasmi ya kumaliza mgogoro huo. Rais wa Korea Kusini Moon Jae in na bwana Kim wanatarajiwa kukutana mwisho wa mwezi Aprili.

Je tunajua nini kuhusu mkutano huo wa kisiri?

Habari kwamba mteule wa rais Donald Trump katika wizara ya maswala ya kigeni alisafiri kueleka Korea Kaskazini kwa mkutano huo na bwana Kim ziliripotiwa mara kwanza na gazeti la The Washington Post.
Ni machache yanayojulikana kuhusu mazungumzo hayo mbali na kwamba yalilenga kuwa jukwaa la kuandaa mkutano mwengine wa moja kwa moja kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un.
Kulingaa na gazeti hilo, mkutano huo ulifanyika mara tu baada bwana Pompeo kuteuliwa kuwa waziri wa maswala ya kigeni kulingana na maafisa wawili waliokuwa na habari kuhusu safari hiyo.
Baadaye chombo cha habari cha Reuters kilisema kuwa ripoti hiyo imethibitishwa na maafisa waandamizi. Ikulu ya Whitehouse haijatoa tamko lolote.

Je Marekani na Korea Kaskazini zinawasiliana vipi?

Marekani haina uhusiano wa kidiplomasia na Korea Kaskazini lakini wajumbe wa mataifa hayo mawili wametembeleana miaka ya mbeleni na kuna idhaa zinazotumika kuwasiliana na Pyonyang.
Safari ya Bwana Pompeo ilikuwa ziara ya ngazi ya juu na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini tangu 2000 wakati waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Madeleine Albright alipokutana na Kim Jong-il, babake kiongozi wa sasa wa Pyonyang.
Mwaka 2014 , kiongozi wa shirika la upepelezi 2014, James Clapper alizuru Korea Kaskazini kisiri ili kujadiliana kuhusu kuwachiliwa huru kwa raia wawili wa Marekani .
Bwana Clapper hakukutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wakati wa ziara hiyo.

Je mkutano huo utafanyika wapi?

Bwana Trump aliishangaza jamii ya kimataifa kwa kukubali mapendekezo ya Pyonyang ya mazungumzo ya moja kwa moja.
Sio kawaida kwa rais wa Marekani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Alisema kuwa mkutano huo utafanyika mwezi Julai ama siku chache kabla ya mwezi huo huku maeneo yakiangaziwa na kwamba hakuna hata eneo moja ambalo liko Marekani miongoni mwao.
Wachanganuzi wamedai kwamba eneo la mazungumzo hayo huenda likawa eneo lisilo na majeshi kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, Beijing, taifa jingine la bara Asia, Ulaya ama hata katika meli iliopo katika maji ya kimataifa.
Kim Jong-un akiwa Pyongyang, Aprili 16Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKim Jong-un ameushangaza ulimwengu kwa kukubali kukumbatia jamii ya kimataifa
Korea Kaskazini imetengwa kwa miongo kadhaa kutokana na historia yake ya unyanyasaji wa haki za kibinaadamu mbali na utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia ikikiuka sheria za kimataifa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Imetekeleza majaribio sita ya kinyuklia na ina makombora ambayo yanaweza kufika Marekani.
Lakini maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi mnamo mwezi Februari nchini Korea Kusini yalitoa dirisha la kidiplomasia na wiki chache baada ya michezo hiyo kumekuwa na ziara kadhaa za Korea kaskazini kutoka China, Korea Kusini na sasa Marekani.

Je habari hii ina uzito gani?

Bwana Trump anakadiria kwamba mkutano huo unaweza kufanyika mwezi Juni ama mapema. Lakini habari za ziara ya bwana Pompeo inatarajiwa kuweka kando uhusiano mzuri kati yake na Japan , ambaye ni mshirika mkuu wa Marekani na jirani wa Korea Kaskazini.
Katibu wa maswala ya habari Ikulu ya Whitehouse Sarah Sanders (kushoto) akishughulikia mkutano kati ya Trump na AbeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKatibu wa maswala ya habari Ikulu ya Whitehouse Sarah Sanders (kushoto) akishughulikia mkutano kati ya Trump na Abe
Kumekuwa na hofu mjini Tokyo kwamba bwana Trump ana mpango wa mazungumzo ya kibiashara ambayo huenda yakaipuuza Japan na Shinzo Abe kwa sasa yuko nchini Marekani kwa mauzngumzo na kiongozi huyo wa Marekani.
Uhusiano kati ya wawili hao ulionekana kuwa mzuri kuhusu swala hilo , ikiwa ni mara ya pili kwamba Trump amemkaribisha bwana Abe katika mgahawa wake wa Mar-a-Lago resort.
Bwana Trump alisisitiza siku ya Jumanne kwamba mataifa hayo mawili yanashirikiana kuhusu swala la Korea Kaskazini , huku naye Shinzo Abe akimpongeza rais huyo wa Marekani kwa kuliangazia swala la Korea Kaskazini.
Hatahivyo waangalizi wanasema kuwa lengo la bwana Abe ziarani Marekani ni kuishawishi Marekani.
Waziri huyo wa Japan ameonekana kutaka kuonyesha uhusiano wa karibu na rais Trump na alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana naye mjini New York baada ya ushindi wake wa uchaguzi wa mwaka 2016.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA