Magufuli asema umma unapotoshwa kuhusu kupotea fedha baada ya ripoti ya CAG


Rais wa Tanzania, Dokta John MagufuliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Tanzania, Dokta John Magufuli
Mjadala kuhusu kupotea kwa fedha nchini Tanzania umechukua sura mpya baada ya Rais wa Tanzania Dokta John Magufuli kuwasimamisha mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na katibu mkuu wizara ya fedha na mipango kueleza kuhusu ukweli wa swala hilo.
Maofisa hao wa serikali waliposimama walikanusha kuwa hakuna upotevu wa fedha hizo
Kwa siku kadhaa sasa nchini Tanzania kumekuwepo mjadala mkali kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali ilibaini utata kuhusu matumizi ya Sh.trilioni 1.5 sawa na dola milioni 650.
Wakati mwanasiasa wa upinzani Zitto Kabwe akitaka ufafanuzi kutoka serikalini kuhusu matumizi ya fedha hizo, viongozi wa chama tawala, CCM na serikali wamekuwa wakisisitiza kwamba hakuna upotevu wowote wa fedha hizo uliotokea.
Mapema leo hii katika hafla ya kuwaapisha majaji wapya ikulu ya Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kinachoendelea kwa sasa ni upotoshaji wa makusudi kwa umma kuhusu sakata hilo
Zitto Kabwe: Kuna tatizo ya namna ambavyo ripoti ya CAG inavyoshughulikiwa
''Siku moja nikampigia CAG mbona kwenye ripoti yako uliyonisomea hapa Ikulu hukunieleza huu wizi wa trilioni 1.5? kwa sababu ungenisomea hapo siku hiyohiyo ningefukuza watu, kama nimefukuza wakurugenzi watatu siku hiyo hiyo kwa sababu ya hati chafu, hawa wa trilioni 1.5 uliwaficha wapi? kwenye ripoti yako sioni, Profesa Assad akaniambia hakuna kitu kama hicho nikamuuliza katibu mkuu akasema hakuna kitu kama hicho''. alieleza rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema hali hii inatokana na uhuru wa watu kusema au kuweka chochote wanachokitaka mitandaoni. Ameonya kwamba hali hii ikiendelea madhara yake kwa taifa ni makubwa.
''Kuna ugonjwa tumeupata watanzania wakufikiri kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli, lakini ni kwa sababu hii mitandao hatui-control sisi wapo watu ambao kazi yao ni kutengeneza biashara'', alisema Rais Magufuli.
Amevitaka vyombo vya sheria kushughulikia kesi za upotoshaji haraka.
Rais Magufuli ameiachia kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kufanya uchunguzi wake.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA