MKIKITA YAUNDA USHIRIKA WA WAKULIMA KUSIMAMIA SHAMBA LA KIWANGWA, BAGAMOYO

 Wajumbe wa Kikosi Kazi cha Ushirika wa Wakulima wa Tanzania Hortcultural Initiatives Society (THIS),  utakaosimamia shamba la pamoja (Block Farming) la Kiwangwa wilayani Bagamoyo, Pwani., wakiwa katika kikao cha kwanza cha kupanga mikakati kwenye Ukumbi wa Anatoglou, Manazi Mmoja Dar es Salaam.
 Ni mwendo mdundo
 Mwenyekiti, Abraham Nyantory,
 Katibu Mkuu Henry Mwizanduru,
 Mweka Hazina, Wombozi Pashua
 Mweka Hazina Msaidizi, Ussi Said Suleiman kutoka Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti Elizabeth Msuya,
 Naibu Katibu Mkuu, Martha Berege

Samwel Timba (Mjumbe)

Na Richard Mwaikenda, Dar

MTANDAO wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), umeanzisha Ushirika wa Wakulima utakaosimamia shamba la pamoja (Block Farming) la Kiwangwa wilayani Bagamoyo, Pwani.

Ushirika huo utakaosajiliwa kwa jina la Tanzania Hortcultural Initiatives Society (THIS), tayari umeunda Kikosi Kazi cha kuratibu usajili na kuifanyia marekebisho Katiba.

Kikosi hicho kinaongozwa na; Mwenyekiti, Abraham Nyantory, Makamu Mwenyekiti Elizabeth Msuya, Katibu Mkuu Henry Mwizanduru, Naibu Katibu Mkuu, Martha Berege,Mweka Hazina, Wombozi Pashua na Mweka Hazina Msaidizi, Ussi Said Suleiman kutoka Zanzibar.

Wajumbe ni;Samwel Timba, Mbarouk Laafify (Zanzibar), Neema Ngowi,Justin Teofil na Mhandisi Francis Macha.Nafasi ya Mwanasheria itajazwa siku za usoni.

Watakaojiunga katika ushirika huo watakuwa wana hiari ya kukodi ama kununua baadhi ya heka za shamba hilo lenye jumla ya heka 250. Kukodi kwa mwaka ni sh. 500,000 na kununua heka moja ni sh. mil. 1. Shamba hilo litakuwa linaendeshwa kwa mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia maji ya Mto Wami ambao uko pembezoni mwa shamba.

Mwanachama ana wajibu wa kulipia kwanza shamba hilo ifikapo Alhamisi Aprili 5, mwaka huu na kulipia pia gharama za awali za uandaaji wa shamba yaani ufyekaji, ung'oaji wa visiki, kulima na mengineyo. 

Malipo haya yafanyike si zaidi ya  Aprili 15 mwaka huu.Kigezo cha kwanza cha kujiunga na ushirika huu ni kulipa  sehemu ya awali ya sh. 30,000 kwa kila mtu, za kusaidia kurekebisha  rasimu ya katiba pamoja na usajili. Gharama kamili itapendekezwa na wajumbe wa Kikosi Kazi katika kikao kitakachofanyika baada ya pasaka.

Wanamkikita na wananchi wengine  wanakaribishwa katika ushirika huu wa kilimo cha papai, mbogamboga na mbegu za muhogo. Mkikita ambayo ndiyo mlezi wa ushirika huo, inawahakikishia wanachama kuwapa utumishi wa heshima ili kuonesha kuwa Tanzania ya Viwanda  itawezeshwa na 
wakulima wa THIS.

Ukitaka Maelezo zaidi, wasiliana kwa namba za simu zifuatazo;Mkikita 0715785869, THIS 
0716507730, 0675149786

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203, 0689425467

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.