NDEGE KUBWA YA ABIRIA YA EMIRATE KUTUA NCHINI YAIPANDISHA TANZANIA KATIKA UTOAJI WA UTOAJI HUDUMA YA USAFIRI WA ANGA


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imesema kuwa kutua kwa Ndege kubwa ya ‘gorofa’ A380 ya Fly Emirates imedhihirisha kuwa uwanja  wa Kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius K Nyerere  na vyombo vyake kuwa madhubuti katika usafiri wa anga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema  kuwa ndege hiyo licha kupata udhuru wa kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mauritius kumeipa heshima nchi katika kuwa na viwango katika utaoaji huduma ya usafiri wa anga.

Amesema kuwa Rubani wa ndege A380 ya Fly Emirates alifanya busara ya kuamua  baada ya kuona hali ya hewa ya Mauritius kutokuwa nzuri na  kuamua kutua kwenye Uwanja wetu wa kimataifa wa Mwalimu Julius  K Nyerere  na kuamini kuwa atatua bila wasiwasi.

Johari amesema kufuatia kutua kwa ndege hiyo kubwa  nchi imeweza kupata mapato katika huduma mbalimbali za kijamii kutokana na abiria waliokuwa katika ndege hiyo zaidi ya watu 500 ambao wote walilala katika hoteli zilizopo nchini.

Amesema kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria duniani ndio mara ya kwanza kutua katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu  Julius K. Nyerere hivyo inaonyesha kujizatiti katika utoaji katika utoaji wa huduma ya usafiri wa anga.

Ndege hiyo imetua Aprili 24 katika uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere ikitokea Dubai ambaye ilishindwa kutua mara tatu katika uwanja wa Mauritius na kuja kutua Tanzania

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa wamekuwa na asilimia  64 kutoka 37 kwa viwango vilivyowekwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) hivyo tuzo yake itatolewa na Rais wa shirika hilo kwa kumkabidhi Rais Dk.John Pombe Magufuli na mawasilino yanafanyika yanafanyika ujio wa Rais wa ICAO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kutua kwa ndege kubwa ya ya Emirate abiria duniani ya A380 ya Ghorofa iliyotua katika uwanja wa Ndege wa Mwalumu Julius Nyerere , jijini Dar es Salaam
Labels: 
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA