Newcastle 2-1 Arsenal: Mapungufu ya Arsenal yaigharimu timu hiyo


Matt Ritchie amefunga bao lake la tatu katika ligi ya England msimu huu dhidi ya ArsenalHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMatt Ritchie amefunga bao lake la tatu katika ligi ya England msimu huu dhidi ya Arsenal
Newcastle imeinyuka Arsenal 2-1 na kuufunga mustakabali wake katika ligi ya England huku jinamizi la rekodi mbaya kwa Arsenal 2018 likiendelea kuiandama timu hiyo ya Arsene Wenger.
Gloi la Matt Ritchie kunako dakika 68th kumeipa timu ya Newcastle ushindi wa nne mtawalia wa ligi na kwa sasa ina pointi 41 huku ikiwa imesalia na michezo 5.
Arsenal, iliyofuzu kuingia katika nusu fainali ya ligi Uropa kwa ushindi wa 6-3 dhidi ya CSKA Moscow nchini Urusi siku ya Alhamisi, inasubiriwa kujinyakulia pointi katika ligi mwaka huu.
Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette, wanaocheza kwa mara ya kwanza pamoja walishirikiana katika bao la ufunguzi la Arsenal kunako dakika ya 14.
Mshambuliaji huyo raia wa Gabon alipokea mchango wake Shkodran Mustafi na kuusukuma mkwaju ndani ya wavu.
bao la Newcastle dhidi ya ArsenalHaki miliki ya pichaREUTERS
Ayoze Perez alilisawazisha muda mfupi kabla ya nusu saa ya mchezo na kukimbia na kumpita Shkodran Mustafi, na kuiogoza krosi ya DeAndre Yedlin karibu na lango kuu.
Calum Chambers alistahili kuisukuma Arsenal mbele kuongoza katika mechihiyo kuelekea mwisho wa nsu ya kwanza ya mechi lakini mpira ulikwenda kombo alipopokea hedi ya Mustafi.
Mambo yalikwenda sare hadi kunako dakika ya 68 wakati Ritchie aliposukuma tobwe la ushindi.
Ilikuwa hali ya roho mkononi kunako dakika zamwisho za mechi hiyo wakatiArsenal ilipokuwa inajizatiti kutoka angalau kwa sare, lakini Newcastle iliendelea kushikilia usukani na kumalizia kwa ushindi huo muhimu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.