RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA DODOMA-BABATI ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikata utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida
kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika
kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika
picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai,
Wabunge pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na Balozi wa Japan hapa
nchini Masaharu Yoshida mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe
kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe
zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na Balozi wa Japan hapa nchini
Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km
251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Mbunge wa Chemba Juma Nkamia mara baada ya kufungua
barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha
Kondoa mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kufungua barabara ya
Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani
Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya
Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya
Dodoma-Babati km 251
Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za
ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani
Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za
ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km
251, Kondoa mkoani Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria
katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251,
Kondoa mkoani Dodoma-PICHA NA IKULU
Comments