TCRA imewapa wamiliki wa blogu Tanzania wiki mbili kujisajili


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA ) imewapa muda wa wiki mbili wamiliki wa mitandao ya kijamii ya 'blogs', tovuti na aina nyingine ya vyombo vya habari vinavyochapisha kwenye mtandao kujisajili nchini Tanzania.
Hatua hii imekuja ili kudhibiti maudhui mitandaoni ikiwa ni matakwa ya sheria mpya ambayo ilionekana kuwa na mkanganyo.
Ikiwa sehemu ya usajili, wachapishaji wote wa kwenye mtandao kwa maandishi, video na sauti wanapaswa kulipa dola 1000.
Haki miliki ya picha Reuters
Aidha wachapishaji wa mtandao huo wanatakiwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote ambavyo wanatakiwa kuainisha ikiwa ni pamoja kuweka mfumo wakukagua taarifa zisozoruhusiwa katika mitandao na kuweka rekodi ya watumiaji wote, vikiwemo vitambulisho vyao na anuani za wasambazaji wa intaneti.
Atakaye kiuka vigezo muhimu vilivyowekwa atapata adhabu ya kulipa faini isiyopungua dola 2000 au kufungwa jela kwa muda usiopungua mwaka mmoja au adhabu zote kwa pamoja.
Wanaharakati wengi, watumiaji wa mtandao na wamiliki wa mitandao hiyo wameona serikali imeamua kutumia mwanya huo ili kubana uhuru wa kujieleza.
Lakini serikali ya Tanzania inasema imeamua kuchukua maamuzi hayo ili kulinda taifa na maudhui kutoka nje au ndani ya nchi ambayo hayahitajiki katika jam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.