Binyavanga Wainaina: Mkenya mpenzi wa jinsia moja kufunga ndoa na raia wa Nigeria


BinyavangaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Mwandishi vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina ambaye ametangaza wazi kwamba ni mpenzi wa jinsia moja amefichua kwamba atafunga ndoa mwaka ujao.
Mwandishi huyo ambaye alifichua hali yake ya kimapenzi mwaka 2014 siku yake ya kuzaliwa akiwa na umri wa miaka 2014 amesema harusi hiyo itafanyika nchini Afrika Kusini.
"Nilimuomba mpenzi wangu tufunge ndoa wiki mbili zilizopita. Na alikubali, karibu mara moja. Yeye ni raia wa Nigeria. Tutakuwa tunaishi Afrika Kusini ambapo atakuwa anahudhuria masomo mwaka ujao. Tutaoana huko, mapema mwaka ujao," Bw Wainaina aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Aliahidi kwamba kutakuwa na karamu kubwa kwa Wakenya jijini Nairobi mwaka ujao.
Baadaye, aliongeza kwamba ana uhakika kutakuwa na sherehe kubwa kwa Wanigeria pia.
"Hakuna lililonishangaza zaidi kuliko kupendana na mtu huyu, ambaye ni mpole na mwenye moyo wa ukarimu.
"Najichukulia kuwa mwenye bahati sana kwamba yeye ananipenda na tulipendana majuzi tu, lakini tumefahamiaka na tumekuwa tunachumbiana tangu 2012."
Bw Wainaina alifichua kuwa yeye ni mpenzi wa jinsia moja mwaka 2014 kwenye makala aliyoipa jina „Mimi ni mpenzi wa jinsia moja, mama."
Presentational grey line

Binyavanga ni nani?

  • Kenneth Binyavanga Wainaina ambaye ana umri wa miaka 47 sasa ni mwandishi wa vitabu na mwanahabari.
  • Mwaka 2002 alishinda tuzo mashuhuri ya uandishi kuhusu Afrika ya Caine.
  • Jarida la Time mwaka 2014 lilimuorodhesha Wainaina kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.
  • Mnamo 1 Desemba, 2016 alitangaza kupitia Twitter Siku ya Ukimwi duniani kwamba alikuwa ana virusi vya Ukimwi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.