Utatazama harusi ya kifalme au fainali kati ya Chelsea na Manchester United kesho Jumamosi



Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamfalme Prince William atakosa kuhudhuria fainali ya kesho kusimamia harusi ya nduguye Prince Harry.
Je wewe utafutilia harusi ya kifalme ambayo itafanyika keshi Jumamosi kati mwanamfalme Prince Harry na Meghan Markle au utatazama mechi ambayo ni fainali ya mechi ya FA kati ya mahasimu Chelsea na Manchester United.
Mwanamfalme Prince William atakosa kuhudhuria fainali hiyo ya kesho Jumamosi kwa kuwa ndiyo siku ya harusi ya nduguye Prince Harry.
Prince William atakuwa msimamizi wa harusi ya nduguye huko Windsor kesho Jumamosi.
William amekuwa rais wa FA tangu mwaka 2006 na mara nyingi ndiye hupeana vikombe na medali.
Mjane wa Ray Wilkins Jackie atatoa kombe hilo kwa washindi huko Wembley.
"Prince William hatahudhuria fainali ya FA kutokana na majukumu kama msimamizi wa harusu ya ndugu yake," alisema msemaji wa Kensington Palace.
Msemaji wa FA alisema: "Tunawatakia Prince William na wale watafunga ndoa siku njema."
Ray Wilkins ambaye alifariki mwezi uliopita akiwa miaka 61, alishinda kombe la FA kama mchezaji wa Manchester United mwaka 1983 na kufunga wakati wa fainali.
Pia alishinda kombe hilo mara tatu akiwa meneja wa Chelsea.

ada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.