UTEKELEZAJI WA BAJETI ZA SEKTA ZA UZALISHAJI NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI


Ndugu zangu:

*Wakulima wa Musoma Vijijini

*Wavuvi wa Musoma Vijijini

*Wafugaji wa Musoma Vijijini


BAJETI za Mwaka wa Fedha wa 2022/2023 za Sekta hizo tatu za UZALISHAJI zimeongezeka sana kwa hiyo tujiitayarishe ipasavyo kwenye UTEKELEZAJI wake. Sisi tuko tayari tunasubiri kuanza kazi tarehe 1.7.2022.


KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA BONDE LETU LA BUGWEMA (Bugwema Irrigation Scheme)


*Jimbo letu linaishukuru sana Serikali kukubali kufufua Mradi wa Bugwema ambao ulikuwa umesahaulika kwa zaidi ya miaka 40.


Bonde letu la Bungwema limewekwa pamoja na eneo lote la MABONDE ya MIKOA ya Ziwa Victoria.


TUME ya UMWAGILIAJI  imetenga TSH BILIONI 2 kufanikisha usanifu na design kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/2023.


Vilevile, Wizara inatafuta fedha kutoka ndani na nje ya nchi, zikiwemo fedha za Sekta Binafsi kwa ajili ya kilimo kikubwa cha umwagiliaji ndani ya mabonde hayo.


Kwa upande wa Bungwema, tumeiambia Wizara kwamba kilimo hicho kinapaswa kuwa na miundombinu ya umwagiliaji itakayotumiwa na makundi yote ya wakulima -  WAKULIMA WADOGO na WAKULIMA WAKUBWA


Vilevile, Bonde hilo ndilo lenye WAFUGAJI wengi na wenye MIFUGO mingi ndani ya Jimbo letu.


Kwa hiyo, masuala ya MALISHO na MAJI kwa mifugo ya Wafugaji wa Bugwema na kwingineko Jimboni mwetu, yatatiliwa mkazo kuepusha migogoro kati ya WAKULIMA na WAFUGAJI.


Mazao makuu yanayopendekezwa kulimwa kwa umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema ni:

*Mpunga

*Mahindi

*Alizeti

*Dengu

*Choroko

*Pamba


UVUVI WA VIZIMBA JIMBONI MWETU


WAVUVI wa Musoma Vijijini wako tayari kuanza UVUVI wa VIZIMBA, kinachokwamisha ni:


Utaalamu

Mitaji ya kutosha


VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAVUVI vya Halmashauri yetu ambavyo vimesajiriwa na VIKO TAYARI kuanza uvuvi wa VIZIMBA ni:


(1) Chama cha Ushirika cha Kurukiri, Kijiji cha Kigera (Etuma)


(2) Chama cha Ushirika cha Busumi, Kijiji cha Bwai Kwituruu


(3) Chama cha Ushirika cha Bwaikumsoma, Kijiji cha Bwaikumsoma


(4) Chama cha Ushirika cha Kasoma, Kijiji cha Kasoma


(5) Chama cha Ushirika cha Kome, Kijiji cha Kome


MIKOPO kwa Vyama  hivyo vya USHIRIKA: tunategemea Wizara ya Uvuvi na Mifugo KUSAIDIA kutafuta vyanzo vya mikopo kwa walengwa hao na kazi ianze tarehe 1.7.2022


SHUKRANI

Wanavijiji wa Vijiji vyote 68 vya Jimbo letu na Viongozi wao wa ngazi zote wanatoa SHUKRANI kwa  nyingi mno kwa SERIKALI yetu chini ya RAIS wetu, Mhe SAMIA SULUHU HASSAN, kwa JITIHADA zinazofanywa za kutafuta FEDHA za MAENDELEO kwetu sisi na kwa Watanzania wengine.


WAWEKEZAJI KWENYE SEKTA ZA UZALISHAJI MNAKARIBISHWA KUWEKEZA MUSOMA VIJIJINI


Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:

www.musomavijijini.or.tz


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz


Tarehe:

Ijumaa, 27.5.2022



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.