KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma Machi 27, 2024.

Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Florent Kyombo wakati kamati hiyo ilipowasili kukagua ujenzi wa jengo hilo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Kyombo wakati  wajumbe wa kamati hiyo walipowasili tayari kwa ajili kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.

Mhandisi wa Mradi SUMA JKT, Baraka Mosha akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo  hilo linalojengwa na SUMA JKT.

Mjumbe wa Kamati hiyo ya Bunge, Yahya Masare (wa tatu kushoto) akisisitiza jambo mbele ya Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mulwambo (kushoto) wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mulwambo akieleza jambo mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Bunge, Abdullah Mwinyi (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Makondo.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mulwambo akifafanua jambo kuhusu maendeleo ya ujenzi huo wakati wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mulwambo akijadiliana jambo na Mjumbe wa Kamati ya Bunge, Mwinyi.

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, SUMA JKT na Washauri wa Ujenzi wa jengo hilo, Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA).

IMEANDALIWA NA RISHARD MWAIKENDA


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI