KIJUE CHUO PEKEE AMBACHO WANAFUNZI WASICHANA HUFUZU WAKIWA BIKIRA


 Kasisi ambaye pia ni mwanzilishi wa chuo kimoja nchini Nigeria amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kwamba chuo chake kina upekee wa aina yake kwani ndicho chuo pekee ambacho wanafunzi wasichana hufuzu wakiwa bado mabikira.

Padre huyo kwa jina Emmanuel Edeh, mmiliki na mwanzilishi wa chuo cha Madonna alisema kwa kujipiga kifua Jumatano kwamba wasichana ambao wanaingia katika chuo hicho wakiwa mabikira hufuzu baada ya masomo yao wangali mabikira vile vile.

Katika video hiyo ambayo imezua maswali mengi kuliko majibu, wengi wakihoji anajuaje kuwa wasichana hao hufuzu wakiwa mabikira, mtumishi wa Mungu aliwataka wanaume wanaotafuta wasichana wa kufunga ndoa nao, basi wasitafute kuingine bali waende katika chuo cha Madonna, ila akaonya kwamba hatokubali hilo hadi pale wasichana wa chuo chake watakapofuzu.

“Ni katika chuo hiki pekee ambapo iko wazi kwamba wasichana ambao wanaingia katika chuo hiki kama mabikira humaliza masomo yao wakiwa mabikira. Unaweza ukaingia katika chuo chetu ukiwa bikira na umalize ukiwa bikira,” mtumishi wa Mungu alisema kwa sauti yenye msisitizo.

“Niambieni chuo chochote duniani ambacho kinaweza kudumisha utamaduni wa aina hii. Hii ndio maana watu kutoka London, Ujerumani, Amerika, wakati ninakutana nao, wananiambia, ‘Padre, ninataka kuoa mwanamke ambaye ni bikira, na mara nyingi huwa hawapati hao mpaka pale wanapokuja chuo cha Madonna,” aliongeza.

Ili kufanikisha hili, kasisi huyo alieleza kwamba wanafunzi wote wa chuo hicho wanaishi katika mabweni na hawaruhusiwi kutoka nje ovyo ovyo.

Kasisi huyo wa kanisa Katoliki pia alisema kwamba mambo kama mafunzo ya itikadi kali, ushoga na wizi wa mitihani hayawezi kusikika wala kupatikana katika chuo hicho.

Kwa mujibu wa tovuti ya chuo hicho mitandaoni, kilianzishwa mwaka wa 1999 na tayari kina matawi matatu katika majimbo ya Anambra, Enugu na River.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI