WAZIRI JAFFO AELEZEA CHIMBUKO, MAFANIKIO LUKUKI YA MUUNGANO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Selemani Jaffo akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma Machi 26, 2024, kuhusu mafanikio mbalimbali ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Wazirti Jafo kuzungumza  na vyombo vya habari.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Msemaji Mkuu wa Serikali, Matinyi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

 Chimbuko la Ofisi ya Makamu wa Rais ni Muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huo ulitokana na Hati ya Makubaliano ya Muungano (Hati ya Muungano) iliyosainiwa na Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, Ikulu Zanzibar tarehe 22 Aprili, 1964.

#Muungano wetu umedumu kutokana na utashi wa dhati wa kisiasa waliokuwa nao Waasisi wa Muungano ambao uliwezesha vyama vya siasa vya TANU na ASP kuungana. Kuunganishwa kwa vyama hivyo kuliongeza ari ya umoja na ushirikiano baina ya watu wa Tanganyika na Zanzibar. 

#Muungano wa vyama hivyo umekuwa ni nguzo muhimu katika kujenga mfumo wa kuwa na vyama vya siasa vya kitaifa na hivyo kukuza demokrasia, uhuru wa kutoa maoni na uwazi katika uendeshaji wa shughuli za kisiasa.

#Mafanikio mengine ya kisiasa ni kutungwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria mbalimbali zinazohusu utekelezaji wa mambo ya Muungano.

#Serikali zote mbili zimefanikiwa kusimamia utekelezaji wa masuala ya Muungano kwa ufanisi mkubwa ikijumuisha kuimarika kwa utaifa, umoja, amani, utulivu na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano. 

#Utekelezaji wa mambo ya Muungano unazingatia Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yale mambo yasiyo ya Muungano yanazingatia sheria, mipango, sera, programu na mikakati ya maendeleo ambayo Serikali zote mbili zimejiwekea kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa Watanzania. 

*MAFANIKIO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA MUUNGANO*

#Shule za Msingi zimeongezeka kutoka shule 3,270 mwaka 1961 hadi shule 20,562 mwaka 2024. Kati ya hizo, shule za Serikali ni 18,012 na za binafsi ni shule 2,550.

#Shule za Sekondari nazo zimeongezeka kutoka shule 41 mwaka 1961 hadi shule 6,511 mwaka 2024. Kati ya hizo, shule 4,892 ni za serikali na 1,619 ni za binafsi. 

#Vituo vya kutolea huduma za afya ngazi zote vimeongezeka kutoka vituo 1,343 mwaka 1960 hadi vituo 9,662 mwaka 2024. Kati ya vituo hivyo, Zahanati ni 8,043; Vituo vya Afya 1,176; Hospitali za Halmashauri 171; Hospitali zenye hadhi ya Wilaya 182; Hospitali za Rufaa za Mikoa 28; Hospitali zenye hadhi ya Mkoa 34; Hospitali za Rufaa za Kanda 5; Hospitali zenye hadhi ya Kanda 11; Hospitali maalumu 6; Hospitali ya Taifa 1; na Hospitali Maalumu za Taifa 6. 

#Upatikanaji wa maji vijijini umeongezeka kutoka asilimia 32 mwaka 2000 hadi asilimia 77 mwaka 2022. Aidha, upatikanaji wa umeme umeongezeka kutoka asilimia 10 mwaka 2000 hadi 78 mwaka 2022. 

#Vile vile, mtandao wa barabara za lami na zege mijini na vijijini umeongezeka kutoka KM 1,360 mwaka 1961 hadi KM 11,966 mwaka 2022.  

#Utoshelezi wa chakula umeongezeka kutoka asilimia 90 mwaka 2000 hadi asilimia 124 mwaka 2022. Vile vile, udugu na uhusiano wa wananchi umeendelea kuimarika ambapo wananchi wa pande zote mbili wameungana katika misingi ya ndoa na kujenga urafiki katika uendeshaji wa shughuli za kibiashara na kijamii.

#Mwenendo wa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha miaka 60 umekuwa ni wa kuridhisha ambapo Pato Ghafi la Taifa limeendelea kukua na kufikia shilingi trilioni 170.3 mwaka 2022 kutoka shilingi trilioni 156.4 mwaka 2021. Aidha, Pato la Taifa kwa mtu limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia wastani wa shilingi 2,844,641 (sawa na dola za Marekani 1,229.1) mwaka 2022 kutoka wastani wa shilingi 2,708,999 (sawa na dola za Marekani 1,173.3) mwaka 2021. 

#Katika kuhakikisha usawa wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Taasisi za Muungano zilizopo Tanzania Bara zimefungua Ofisi Zanzibar ambapo hadi sasa Taasisi 33 zimefungua Ofisi Zanzibar kati ya Taasisi 37 za Muungano.

#Tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa vikao vya pamoja mwaka 2006 hadi sasa, kasi ya utatuzi wa changamoto imeongezeka ambapo hoja 22 zimepatiwa ufumbuzi kati ya hoja 25 zilizoibuliwa.

#Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 pekee, hoja 15 zimepatiwa ufumbuzi kati ya hoja 18 zilizokuwepo kwa kipindi hicho. 

#Miongoni mwa miradi na programu zilizotekelezwa na kukamilika katika pande mbili za Muungano ni pamoja na: miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu ya I hadi III; Programu ya Usimamizi wa Bahari na Pwani (MACEMP) na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP).

#Programu zingine ni, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Sekta ya Mifugo (ASDP  L); Programu ya Kuwezesha Sekta ya Kilimo (ASSP); Programu ya Changamoto za Milenia (MCA  T); Mradi Shirikishi wa Programu za Maendeleo ya Kilimo (PADEP); na Mradi wa Udhibiti wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH).

#Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani ya Mazao na uboreshaji wa huduma za Fedha Vijijini (MIVARF); Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa Zao la Mpunga (ERPP); Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Maeneo ya Pwani (LDCF); na Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Uhakika na Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame ya Tanzania.

#Programu na miradi inayoendelea kutekelezwa pande mbili za Muungano ni pamoja na: miradi ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDCF); Mradi wa Ujenzi wa Kingo za Kuzuia Maji ya Bahari; na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia ya Vijijini (EBARR).

#Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2022, takribani shilingi bilioni 1.4 zimekuwa zikipelekwa Zanzibar kila mwaka na kuanzia mwaka 2023 shilingi bilioni 1.75 na kwa mwaka 2024 shilingi 2,034582,000 zimekuwa zikipelekwa Zanzibar kila mwaka na kufanya jumla fedha zilizopelekwa Zanzibar kwa kipindi hicho kuwa shilingi 20,874,314,940.00.00.

#Ofisi ya Makamu wa Rais (SJMT) kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ), zimeweka Mwongozo wa Vikao vya Kuimarisha Ushirikiano, tathmini inaonesha Wizara za Kisekta zinapokutana changamoto zinapungua na Muungano unazidi kuimarika. Jumla ya vikao 242 vya ushirikiano vimefanyika katika kipindi cha 2010 - 2024. 

#Katika utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, jumla ya Sheria Ndogo 326 zimeandaliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa ya Dodoma (15), Kilimanjaro (7), Mbeya (57), Mtwara (69), Morogoro (53), Pwani (59) na Ruvuma (66).

#Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3.3 ulitekeleza mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi kwa wataalam zaidi ya (80) wa Halmashauri za wilaya ya Rufiji, Pangani, Bagamoyo pamoja na Zanzibar.

#Shughuli nyingine zilizotekelezwa na mradi huo ni pamoja na upandaji wa hekta 1,250 za miti ya mikoko; ujenzi wa ukuta wa Kisiwa Panza-Pemba wa mita 40; ujenzi wa ukuta wa Pangani wa mita 950; ujenzi wa makinga bahari matano (5) yenye urefu wa mita 100 kila moja katika eneo la Kilimani-Unguja ili kuzuia mmomonyoko wa fukwe za bahari katika maeneo hayo.

#Miradi mingine inayoendelea kutekelezwa katika upande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Uhakika na Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame ya Tanzania (LDFS) ambao unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

#Lengo la mradi huo ni kuboresha usimamizi endelevu na kuwezesha urejeshwaji wa mifumo ikolojia iliyoharibika inayochangia kutoa huduma muhimu za uzalishaji kwenye maeneo ya ardhi, maji, misitu na bionuai kwa madhumuni ya kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula,

#Mradi mwingine ni wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBBAR), lengo la mradi ni kuongeza uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii za vijijini kwa kuimarisha mifumo ikolojia na shughuli mbadala za kujiongezea kipato.  

#Natoa rai kwa wananchi wote wa Tanzania kuendelea kuuenzi na kuutunza Muungano wetu adhimu ambao umedumu kwa miaka 60. Huu ni muungano wa kipekee barani Afrika na duniani kwa ujumla.
*Aliyosema Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi*

#Kupitia mikutano hii ya kuelekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Mawaziri ambao wanasimamia wizara zenye taasisi za Muungano wanapata fursa kuja kuzungumza na watanzania kuelezea tulipotoka, tulipo na tunapokwenda.

#Katika kipindi hiki cha shamrashamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano, wataalam kutoka taasisi za Muungano watapata fursa ya kupita katika vyombo mbalimbali vya habari kuelezea masuala mbalimbali ya Muungano yanayofanywa na Serikali.

#Baada ya Muungano wetu Aprili, 1964, watanzania tuliendelea kutafuta jina litakaloifaa nchi yetu, ilipofika mwezi Oktoba, jina Tanzania likazaliwa. Kabla ya hapo nchi ilijulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

#Tunapenda kukumbuka historia yetu na kuwashukuru viongozi wetu ambao ni waasisi wa Muungano, Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Aman Karume.

#Tunaposherehekea miaka 60 ya Muungano, tuna kila sababu ya kujivunia historia yetu tukiwa ndio Jamhuri ya Muungano pekee iliyofanikiwa katika bara la Afrika kwani nchi nyingine zilijaribu lakini hawakumudu.

#Natoa wito kwa Waandishi wa Habari na kuwaomba ushirikiano wenu katika kipindi hiki cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO*
[3/26, 12:45 PM] Jack Maelezo: *YALIYOJIRI LEO MACHI 26, 2024 JIJINI DODOMA WAKATI WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA),  MHE. DKT. SELEMANI JAFO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.* 

*Aliyosema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo*

#Chimbuko la Ofisi ya Makamu wa Rais ni Muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huo ulitokana na Hati ya Makubaliano ya Muungano (Hati ya Muungano) iliyosainiwa na Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, Ikulu Zanzibar tarehe 22 Aprili, 1964.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI