CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA


 KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla anatarajia kuanza ziara ya siku nne katika Mkoa wa Arusha kuanzia Septemba 4 hadi 7 mwaka huu.

CPA Makalla atawasili mkoani humo Septemba 4, ambapo kama ratiba Inavyoonesha atafanya mikutano mikubwa ya hadhara katika Wilaya za Longido, Ngorongoro, Karatu na Monduli.

Pamoja na mambo mengine atakayoyafanya katika ziara hiyo,  CPA Makalla  atakagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

MAMILIONI YA CCM YATUA AKAUNTI YA TUNDU LISSU

ASKOFU CHANDE AISHUKURU SERIKALI KULIPATIA USAJILI WA KUDUMU KANISA LA KARMELI

"WANAUME WAPO GEREZANI, KABURINI"

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA