TANZANIA HAICHAGUI MARAFIKI WA KUTEKELEZA DIRA 2050 - PROF MKUMBO

 


NA MWANDISHI WETU

TANZANIA imepanga kuendelea kutafuta wadau katika kila pembe ya dunia ili kutekeleza Dira ya 2050 na kupata matokeo chanya kwa maslahi mapana ya Taifa.

Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji amebainisha hayo leo Juni 7, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari.


Waziri Prof. Mkumbo katika mkutano huo ambao ulikuwa mahusus kuelezea matokeo ya safari ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan iliyofanyika nchini Urusi, alifafanua kwamba katika kusaka mafanikio Tanzania haitachagua marafiki wa kufanya nao kazi.

Pia akijibu swali la Tanzania itawezeke kufanya kazi na Urusi kutokana na kuelewa vikwazo, alifafanua kwamba mataifa yote Duniani inashirikiana na Urusi kidiplomasia hivyo haizuii kushirikiana nayo katika masuala ya kiuchumi, hivyo Tanzania haitachagua marafiki wa kufanya nao kazi kutekeleza Dira ya 2050.

Aidha, amebainisha kuwa katika ziara hiyo, Tanzania na Urusi zimekubaliana kushirikiana katika maeneo tisa ambayo ni kilimo, elimu na mafunzo, nishati, madini, viwanda, usafiri na usafirishaji, utalii, uchumi wa kidijitali pamoja na biashara na uwekezaji.


Pia amesema kuwa ushirikiano huo tayari umeanza kuzaa matunda kupitia kutiwa saini kwa hati nane za makubaliano, ikiwemo makubaliano kati ya Chuo Kikuu cha Mzumbe na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ya kuendeleza lugha za Kiswahili na Kirusi katika nchi hizo mbili. Aidha, amebainisha kuwa lugha ya Kirusi itaanza kufundishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Pia mataifa hayo yamesaini makubaliano kati ya Wizara ya Elimu ya Tanzania na Wizara ya Elimu ya Juu ya Shirikisho la Urusi kuhusu ushirikiano katika masuala ya elimu ya juu, sayansi, teknolojia na ubunifu.


Pia ameongeza kuwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Maalum Tanzania (TISEZA), Tanzania imefanikiwa kuvutia uwekezaji katika maeneo ya madini, utalii, kilimo, uzalishaji wa dawa, miundombinu, mbolea na sekta ya fedha. 





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

NGUVU YA UJASUSI WA TANZANIA KITOVU CHAKE NI IRINGA TANGU ENZI ZA MKWAWA