RAIS SAMIA AUNGANA NA VIONGOZI WENGINE KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA WANAHISA

Leo jijini Dar es Salaam nimeungana na viongozi wengine wa Afrika kufungua Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika, ambapo Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji. Jukwaa hilo, linaloadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, limekuwa sehemu muhimu ya kuunganisha mitaji, miradi na wataalamu ili kuharakisha maendeleo ya miundombinu barani Afrika.


Katika mkutano huo nimeeleza kuwa, Tanzania inashirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuimarisha miundombinu, ikiwemo barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege. Hatua hii inachochea ukuaji endelevu wa uchumi kwa kupunguza gharama za usafirishaji, kukuza biashara, kuvutia uwekezaji, kutoa ajira na kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha usafirishaji.


Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kimazingira duniani, nimesisitiza umuhimu wa Afrika kuimarisha miundombinu inayohimili mabadiliko hayo na kuunganisha nchi zetu ili kuendelea kukuza biashara, uwekezaji na uongezaji thamani wa rasilimali zetu.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAAFISA JENERALI WASTAAFU 17 WA JWTZ WAAGWA.

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

HII NDIYO CV YA KOCHA MPYA WA YANGA

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

CDF MKUNDA AWATAKA MAAFISA JENERALI WASTAAFU KUACHA KUHANGAIKA NA SIASA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII