NECTA YATANGAZA MTIHANI WA DARASA LA SABA SEPTEMBA 9 NA 10


 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza kuwa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mwaka 2026 utafanyika Septemba 9 na 10, ukihusisha watahiniwa 1,168,649 kutoka shule 20,019 nchini.


Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said A. Mohamed, amesema kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 531,467 sawa na asilimia 45, huku wasichana wakiwa 637,182, sawa na asilimia 55.


Amesema watahiniwa 1,081,204, sawa na asilimia 93, watafanya mtihani huo kwa kutumia lugha ya Kiswahili, wakati watahiniwa 87,445, sawa na asilimia saba, watafanya kwa lugha ya Kiingereza.


Kwa mujibu wa Prof. Mohamed, watahiniwa wenye mahitaji maalumu 4,867 wamesajiliwa kufanya mtihani huo.


Amesema kati ya watahiniwa hao, 82 ni wasioona, 1,591 wana uoni hafifu, 999 wana uziwi, 576 wana ulemavu wa akili, huku 1,619 wakiwa na ulemavu wa viungo.


Masomo yatakayotahiniwa ni Kiswahili, English Language, Sayansi na Teknolojia, Hisabati, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi, pamoja na Uraia na Maadili.


Prof. Mohamed amesema Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi wa mwaka 2026 utakuwa wa mwisho kufanyika kwa kutumia mtaala wa sasa.


Ameeleza kuwa mtihani huo unalenga kupima maarifa na ujuzi walioupata wanafunzi katika kipindi cha miaka saba ya elimu ya msingi, pamoja na kutumika katika mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na elimu ya sekondari.The National Examinations Council of Tanzania Mount Kibo Schools

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA