MABAUNSA MARUFUKU KULINDA WAGOMBEA

Na Richard Mwaikenda

WAGOMBEA ubunge na udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi

(CCM), wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuwatumia

mabaunsa kuwalinda, badala ya Green Guard wanaotakiwa

kufanya kazi hiyo.


Tamko hilo lilitolewa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya

Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Ridhiwani

Kikwete wakati wa mkutano wa ndani wa kampeni za kuweka

mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM katika uchaguzi

ujao,uliofanyika Kigamboni, Dar es Salaam juzi.



"Hivi sasa kuna tabia imezuka kwa  wagombea hao kuwatumia

walinzi wao binafsi (mabaunsa) kuwalinda badala vijana wetu

wa Green Guard.Naomba tabia hiyo ife mara moja,"alifoka

Ridhiwani huku akipigiwa makofi.


Tabia hiyo ya wagombea kulindwa na mabaunsa ilionekana

katika mikutano mbalimbali ya kampeni, ikiwemo ya Kata ya

Kijitonyama, Kawe na Kigamboni Dar es Salaam.


Alisema wagombea hao wanapaswa kufuata utaratibu wa chama

kwa kuwatumia  vijana wao wa Green Guard ambao ni makada wa

chama hicho waliopata mafunzo maalumu kwa ajili ya kuwalinda

wagombea na mikutano ya kampeni.


Alisema si vizuri kuwatumia mabaunsa kwani asilimia kubwa si

makada hivyo hawawezi kutunza siri cha chama zinazozungumzwa

wakati wa mikutano ya ndani ya kampeni.


CCM, iliwandaa vijana wa Green Guard kutoka mikoa mbalimbali

nchini katika kambi iliyofanyika Ihemi Iringa, kwa ajili ya

kulinda viongozi, wagombea na mikutano ya chama.



mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.