Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Jamii kuondokana na dhana ya kwamba Mwanamke ni mnyonge anayetakiwa kusaidiwa bali apewe nafasi kutokana na Uwezo wake.
Aidha, amesisitiza Viongozi Wanawake kuondokana na mtazamo wa kwamba wao pia ni wahanga wa ubaguzi wa kijinsia bali waongeze ujasiri na jitihada za kukabiliana na changamoto wanazopitia, ili kuwahamasisha mabinti na watoto wakike kujitambua kuwa wao pia wanaweza.
Dkt. Tulia ameyasema hayo wakati akishiriki katika Mkutano wa Jukwaa la Kibunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-PF) unaoendelea leo tarehe 3 Julai, 2024 Luanda nchini Angola.
Comments