BODI YA STAKABADHI YA GHALA YAELEZA MAFANIKIO YAKE KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Kilimo, Deodatus Mwanyika akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu akielezea kuhusu utendaji, mafanikio na changamoto zinazoikabili bodi hiyo, wakati wa kikao na wajumbe wa kamati hiyo katika moja ya kumbi za mikutano za Bunge jijini Dodoma Oktoba 23, 2024.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwanyika akiongoza kikao hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu akielezea kuhusu utendaji, mafanikio na changamoto zinazoikabili bodi hiyo wakati wa kikao na wajumbe wa kamati hiyo katika moja ya kumbi za mikutano za Bunge jijini Dodoma Oktoba 23, 2024.

Bodi hiyo ambayo iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, kazi yeke kuu ni kusimamia na kuhamasisha matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani unaohakikisha usawa na uendelevu wa upatikanaji wa mikopo na mifumo ya masoko.

Dhamira yake ni Kuchochea maendeleo ya uchumi wa bidhaa na wamiliki wa ghala kwa kusimamia ghala na kuhakikisha usawa na upatikanaji endelevu wa huduma za fedha, mifumo ya masoko ya mazao na bei ya ushindani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Jaffo akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wakiwa makini kusikiliza uwasilishwaji huo.


Baadhi ya maafisa wa wizara hiyo na bodi hiyo wakiwa katika kikao hicho.
Waziri Jaffo akiandika baadhi ya mambo muhimu.
Waziri Jaffo akiwa na viongozi wa wizara na bodi wakiondoka baada ya kikao kumalizika.


 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MSIMAMIZI MKUU

KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV

0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO

NDOGO WA MUME WANGU ALIKUWA EX WANGU