Leo, Baraza la Jumuiya ya Wazazi la Wilaya ya Musoma Vijijini limemtunuku Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, TUZO ya PONGEZI kwa kutambua ushiriki wake na mchango wake mkubwa wa fedha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika tarehe 27.11.2024
Kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Musoma Vijijini:
Mgeni Rasmi: Ndugu Simon Rubugu
Katibu wa Siasa, Mwenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Mara
Ushiriki wa Prof Muhongo kwenye Uchaguzi:
*Kuelezea wananchi (wapiga kura) mafanikio makubwa ya Serikali yetu inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
*Kuelezea wananchi (wapiga kura) mafanikio makubwa yanayopatikana Jimboni mwetu kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025
*Kuelezea wananchi (wapiga kura) vipaumbele vya sasa na vya miaka ijayo vya mahitaji ya wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini
Kutoa michango mikubwa ya fedha kugharimia:
(i) uchapishaji na ugawaji wa vitabu viwili vya rangi (Volumes III & IV) vinavyoelezea miradi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimboni mwetu - nakala elfu moja na mia tano (1,500)
(ii) posho za mawakala wakati wa upigaji kura za maoni ndani ya Chama chetu (CCM), matawi 95
(iii) usafiri kwenye kampeni za wagombea wa CCM nafasi za Serikali za Vijiji 68,
(iv) usafiri wa wapiga kampeni wakiwemo viongozi watatu kutoka kila Kata (jumla: Kata 21)
(v) magari manne (4) yaliyotumiwa kwenye kampeni,
(vi) usafiri wa boti (mafuta & posho) kwenda kwenye kampeni za visiwa vitatu (3) vikubwa
(vii) posho za washiriki mbalimbali wa kampeni, n.k.
Ushiriki wa Viongozi wa Chama:
Viongozi wa Chama (CCM) na Jumuiya zake (WAZAZI, UWT na UVCCM) ngazi za Wilaya, Kata, Matawi walishiriki kwa kujituma ipasavyo hadi kupata ushindi mkubwa kwenye Uchaguzi huo:
(i) Vijiji 68: CCM 66 (97.06%), CHADEMA 2
(ii) Vitongoji 374: CCM 358 (95.72%), CHADEMA 16
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Matukio mbalimbali ya utoaji wa TUZO ya PONGEZI kwa Prof Sospeter Muhongo. Hii ilikuwa leo, kwenye Kikao cha Baraza la Wazazi wa Wilaya ya Musoma Vijijini kilichofanyika Kijijini Murangi.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumanne, 17 Dec 2024
Comments