1. Idadi ya Sekondari Jimboni mwetu:
(Kata 21 zenye Vijiji 68)
1a. Sekondari za Kata/Serikali: 26
1b. Sekondari za Madhehebu ya Dini: 2
1c. "High Schools": 1
1d. "High Schools" mpya za sayansi: 2
*Malengo ya Musoma Vijijini:*
*Kila kijiji kiwe na Shule za Msingi za kutosha
*Kila kijiji kiwe na Sekondari moja
2. Sekondari mpya zitakazofunguliwa 2025
2a. Zinazojengwa na Serikali: 3
(Vijijini: Butata, Kasoma & Kurwaki)
2b. Zinazojengwa na wanavijiji: 3
(Vijijini: Muhoji, Nyasaungu &
Kisiwani Rukuba)
3. Sekondari mpya zilizoanzwa kujengwa mwaka huu (2025) kwa nguvu za wanavijiji: 6
3a. Chitare Sekondari, Kata ya Makojo
3b. Mmahare Sekondari, Kata ya Etaro
3c. Kataryo Sekondari, Kata ya Tegeruka
3d. Nyabakangara, Kata ya Nyambono
3e. Mwigombe Tech, Kata ya Kiriba
3f: Musanja Sekondari, Kata ya Musanja
Fedha za Mfuko wa Jimbo:
Kila moja ya hizo sekondari sita (6) tayari imepewa Saruji Mifuko 150, na nyingine zimepewa nondo
4. HARAMBEE ZA MBUNGE:
Mbunge wa Jimbo ameishapiga Harambee za kutafuta vifaa vya ujenzi wa sekondari zifuatazo:
4a: Chitare: mifuko ya saruji
Wanakijiji 50, Mbunge 150
4b. Mmahare: mifuko ya saruji
Wanakijiji 155, Mbunge 155
4c. Mwigombe Tech: mifuko ya saruji
Wanakijiji 182, Mbunge 200
Familia Mashenene: inajenga darasa
Mbunge wa Jimbo ameanza kutoa mifuko ya saruji (ahadi zake binafsi) kwa vijiji vilivyoanza ujenzi unaonekana na kufuatiliwa ipasavyo.
4d. Tarehe za Harambee zijazo:
*Nyabakangara Sekondari, Kijijini Nyambono
Tarehe 25 Machi 2025
Saa 8 mchana
*Kataryo Sekondari, Kijijini Kataryo
Tarehe 26 Machi 2025
Saa 8 mchana
*Musanja Sekondari, Kijijini Musanja
Tarehe 27 Machi 2025
Saa 8 mchana
VIDEO/CLIP iliyoambatanishwa hapa inaonesha:
Wanakijiji wakiwa kazini Kijijini Chitare, Kata ya Makojo. Matofali 3,750 tayari yamefyatuliwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chitare Sekondari. Hii ni sekondari ya pili ya Kata hii ya Makojo.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumamosi, 15 Machi 2025
13:00 hrs
Comments