TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI MACHI 16, 2025

Liverpool wanatazamiwa kuzishinda Chelsea na Newcastle United katika usajili wa majira ya kiangazi wa Marc Guehi wa Crystal Palace, 24, huku Anfield ndio mahali anapopendelea mlinzi huyo wa Uingereza. (Mirror)

Wakala wa mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez anasema Liverpool ilimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kabla ya kujiunga na Atletico Madrid kutoka Manchester City msimu uliopita. (Winwin via Liverpool Echo)

Liverpool wanaweza kufikiria kumuuza mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez msimu wa joto, huku meneja wa Arsenal Mikel Arteta akiaminika kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes)

Real Madrid itafanya jaribio la kumnunua beki wa Arsenal Mfaransa William Saliba, 23, msimu wa joto. (Relevo)

Manchester United, Liverpool na West Ham wanavutiwa na mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 25, ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto. Lakini vilabu vya Premier League vinakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona, Juventus na Inter Milan. (Tuttojuve)

Newcastle United na Aston Villa wanaongoza katika kinyang'anyiro cha uhamisho wa mshambuliaji wa Besiktas mwenye umri wa miaka 19, Semih Kilicsoy, ambaye pia amevutiwa na Fulham, Everton na Nottingham Forest. (Caughtoffside)

Sunderland wanaweza kuangalia ofa zaidi ya pauni milioni 20 kwa kiungo wa kati wa Uingereza Jobe Bellingham ikiwa hawatapandishwa kutoka kwenye michuano hiyo, huku Borussia Dortmund, Chelsea, Crystal Palace na Tottenham zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Football Insider)

Timo Werner, 29, huenda akajiunga na New York Bulls kwa mkopo kutoka klabu dada ya RB Leipzig msimu wa joto, baada ya Tottenham kuchagua kutochukua chaguo la kumnunua mshambuliaji huyo wa Ujerumani. (Team talk)


 Mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic anasema anataka kusalia AC Milan huku kukiwa na uvumi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Italia. (Soka Italia)

Meneja wa Liverpool Arne Slot amedokeza kuwa mlinda mlango wa Brazil Alisson Becker, 32, ataanza fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Newcastle United Jumapili badala ya Caoimhin Kelleher wa Jamhuri ya Ireland. (Independent).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA