uchaguzi mkuu mwaka huu ,Wasira amewataka wananchi wakiwemo wa Wilaya ya Ngara kujiandaa na uchaguzi huo na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuzuia uchaguzi usifanyike maana amewasikia CHADEMA wakiendelea na kauli yao ya No Reforms No Election lakini ukweli hakuna wa kuzuia uchaguzi mkuu.
KUHUSU WAPINZANI
Akizungumza kuhusi upinzani alisema wako watu wanauliza kwa nini CCM bado inaendelea kutawal kwa kuwa hawajui historia.
"Siku moja nilikuwa na balozi mmoja akaniuliza CCM mnashindaje uchaguzi asilimia 99, nikamwambia huko vijijini hakuna upinzani.
"Ndio maana walikosa wajumbe hata wa kusimamisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa tuwasaidieje nikamuuliza.
"Asilimia 60 ya wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa walikuwa wa CCM, vyama vya upinzani havina watu na ushahidi upo mpaka kwenye vijiji vya ngara hapa hawapo," alieleza.
Comments