UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI NA UANZISHWAJI WA "HIGH SCHOOLS" ZA SAYANSI*


Musoma Vijijini- kila Sekondari inapaswa kuwa na maabara tatu za masomo ya sayansi. Masomo hayo ni yale ya Fizikia, Kemia na Bailojia


Jimbo letu linao mradi kabambe wa ujenzi wa maabara hizo tatu kwa kila Sekondari ya Kata.


Wanavijiji na Viongozi wao wanashirikiana na Halmashauri yetu (Musoma DC), na Serikali Kuu kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye Sekondari zetu za Kata.


Malengo ya ujenzi wa maabara hizi:


(i) kuboresha ufundishaji, ujifunzaji, uelewa na ufaulu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa Jimboni mwetu


(ii) Uanzishwaji wa "High Schools" za masomo ya sayansi Jimboni mwetu. 


Kwa sasa tunayo "High School" moja tu nayo ni ya masomo ya "arts"- Kasoma High School.


Wizara imetoa kibali cha kufunguliwa "High Schools" mpya mbili za masomo ya sayansi, ambazo ni: Suguti na Mugango High Schools


*Idadi ya maabara za masomo ya sayansi Jimboni mwetu:*


(i) Sekondari zenye maabara tatu: 6

(ii) Sekondari zenye maabara mbili: 8

(iii) Sekondari zenye maabara moja: 4

(iv) Sekondari zisizo na maabara: 8


(v) Sekondari za Madhehebu ya Dini

       Nyegina (maabara 2), Bwasi (2)


*Sekondari zisizokuwa na maabara (8):*

*Bukwaya (Kata ya Nyegina)

*Busambara (Busambara)

*Ifulifu (Ifulifu)

*Murangi (Murangi)

*Mtiro (Bukumi)

*Nyanja (Bwasi)

*Seka (Nyamrandirira)

*Tegeruka (Kata ya Tegeruka)


*Tunaombwa tuchangie ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye sekondari hizo nane*


*Sekondari zenye maabara moja (4):*

*Bukima (Kata ya Bukima)

*Dan Mapigano Memorial Sec (Bugoji)

*Mabuimerafuru (Musanja)

*Kasoma (Kata ya Nyamrandirira)


*Tunaombwa tuchangie ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye sekondari hizo nne*


*Mtiro Sekondari: ujenzi wa maabara*


Wachangiaji wa ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi ya Mtiro Sekondari ya Kata ya Bukumi (vijiji: Buira, Bukumi, Buraga na Busekera)


(i) Wanavijiji

(ii) Mbunge wa Jimbo

(iii) Mfuko wa Jimbo

(iv) Halmashauri yetu (Musoma DC)


Mtiro Sekondari inakaribia kukamilisha vigezo vya kuanzishwa kwa "High School" ya masomo ya sayansi:


*Maji ya bomba: yapo

*Umeme: upo

*Bweni la wanafunzi: lipo

*Maabara: zinajengwa (picha) 


Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:

Maboma ya maabara tatu za masomo ya sayansi ya Mtiro Sekondari ya Kata ya Bukumi 


Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la Musoma Vijijini 

www.musomavijijini.or.tz 


P. O. Box 6

Musoma 


Tarehe:

Jumatatu,17 Machi 2025


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69