WAFANYABIASHARA WA MBOLEA WAMEONGEZEKA HADI 7302 - TFRA

 KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita,inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, biashara ya mbolea nchini imekua kwa kiasi kikubwa ambapo wafanyabiashara wa mbolea waliopewa leseni wameongezeka kutoka 3,069 mwaka 2020/21 hadi 7,302 Februari, 2025.


 Aidha, upatikanaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 766,024 mwaka 2020/2021 hadi tani 1,213,729 mwaka 2023/2024, uingizaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 504,122 mwaka 2020/2021 hadi tani 728,758 mwaka 2023/2024 na uzalishaji wa ndani umeongezeka kutoka tani 42,695 mwaka 2020/2021 hadi tani 158,628 mwaka 2023/2024.


Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita  Machi 19, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.


Ametaja mafanikio mengine kuwa ni Kutokana na kuongezeka kwa viwanda vya kuzalisha mbolea na visaidizi vya mbolea kutoka viwanda 16 mwaka 2020/2021 hadi viwanda 33 mwaka 2023/2024. Kati ya viwanda hivyo, vitatu (3) ni vikubwa,  viwanda 11 ni vya kati na viwanda 19 ni vidogo.


"Taifa limeshuhudia ongezeko la matumizi ya mbolea kutoka tani 363,599 mwaka 2020/2021 hadi tani 840,714 mwaka 2023/2024. Ongezeko hilo limewezesha kuongezeka kwa matumizi ya mbolea kutoka kilo 19 za virutubisho kwa hekta mwaka 2020/2021 hadi kilo 24 za virutubisho kwa hekta mwaka 2024/2025


 Lengo ni kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta ifikapo mwaka 2033 kwa kuzingatia makubaliano ya Wakuu wa Nchi za Afrika yaliyofanyika Nairobi 2024,"amesema Laurent.

 

Amefafanua kuwa kuongezeka kwa matumizi ya mbolea nchini kumechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 19,980,718 mwaka 2020/2021 hadi tani 22,803,316 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 14 na kufanya utoshelevu wa chakula nchini kufikia asilimia 128.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent alipokuwa akizungumza katika mkutano huo.

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MSIMAMIZI MKUU 
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA