Baada ya kutoridhishwa na majibu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), klabu ya Yanga SC leo jioni imewasilisha rasmi malalamiko yake katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).
Yanga SC imeeleza kutokuwa na imani na Bodi ya Ligi (TPLB) na haijakubaliana kabisa na majibu yaliyotolewa na TFF. Kutokana na hali hiyo, klabu hiyo imeamua kuchukua hatua zaidi kwa kuipeleka kesi hiyo CAS ili kudai haki yao.
Kwa sasa, malalamiko hayo tayari yamewasilishwa, na kinachosubiriwa ni taratibu za usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo.
Comments